Shirikisho la Mikronesia

Shirikisho la Mikronesia ni nchi ya visiwani katika Bahari Pasifiki iliyoko kaskazini kwa Papua Guinea Mpya.

Shirikisho la Mikronesia

Ni nchi huru inayoshirikiana na Marekani. Nchi ilikuwa eneo lindwa chini ya Marekani kwa niaba ya Umoja wa Mataifa hadi ikapata uhuru wake mwaka 1986.

Jiografia hariri

Shirikisho linajumlisha sehemu kubwa ya funguvisiwa la Karolini katika Mikronesia, kanda la Pasifiki. Jumla ya visiwa ni 607.

Nchi ina majimbo manne ya kujitawala ambayo ni Chuuk, Kosrae, Pohnpei na Yap.

Visiwa vya Palau pia ni sehemu ya Karolini lakini ni nchi ya pekee.

Mji mkubwa wa nchi ni Weno (wakazi 17,624) kisiwani Chuuk lakini mji mkuu ni Palikir kwenye kisiwa cha Pohnpei.

Majimbo ya shirikisho hariri

Kuna majimbo manne kama yafuatayo:

Bendera Jimbo Mji Mkuu Eneo la nchi kavu[1] Wakazi[2] Msongamano
  Chuuk Weno 127 km2 53,595 1,088 per km2
  Kosrae Tofol 110 km2 7,686 70 per km2
Pohnpei Palikir 346 km2 34,486 100 per km2
  Yap Colonia 118 km2 11,241 95 per km2

Historia hariri

 

Visiwa vimekaliwa na watu tangu miaka 4,000 iliyopita, hasa kutoka Rasi ya Malay na visiwa vya Indonesia. Wengine wametokea visiwa vya Polinesia.

Kisiwani Yap kulitokea dola na utawala wa kifalme.

Tangu kufika kwa Wahispania katika karne ya 16 visiwa vilikuwa chini ya ubwana wa nje lakini maisha ya kawaida yaliendelea bila mabadiliko makubwa kwa muda mrefu.

Mwisho wa karne ya 19 Hispania iliuza koloni hilo kwa Ujerumani; utawala wa Kijerumani ulikwisha katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ukachukuliwa na Japani hadi mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Japani ilifuatwa na Marekani iliyoendelea kutawala kwa niaba ya UM hadi uhuru.

Lugha na utamaduni hariri

 
Kanisa katoliki kisiwani Pohnpei

Kuna lugha 18 ambazo huzungumzwa katika Shirikisho la Mikronesia. Lugha rasmi ni Kiingereza.

Wakazi wengi ni wa makabila ya asili.

Upande wa dini, wengi ni Wakristo (95.3%), kwanza Wakatoliki (52.6%) halafu Waprotestanti wa madhehebu mbalimbali (41.7%).

Uchumi hariri

Uchumi wa nchi hutegemea hasa kilimo cha kujisukuma na uvuvi. Mapato ya serikali ni kutokana na vibali kwa wavuvi wa nje wanaovua samaki ndani ya maji ya shirikisho.

Kuna pia uchimbaji wa fosfeti.

Shirikisho la Mikronesia pamoja na Nauru vinaongoza duniani kwa asilimia kubwa ya watu wanene.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. "FSM government website - Geography". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2007-04-07. 
  2. "FSM government website - Population". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-06-29. Iliwekwa mnamo 2007-04-07. 


  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.