Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake.[1] Kampeni hii hufanyika kuanzia tarehe 25 Novemba na kumalizika tarehe 10 Desemba ya kila mwaka kwa ajili ya kupinga ukatili na kutetea haki za wanawake.

Watoto wakiwa katika moja ya maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia, Arusha, Tanzania.

Siku hiyo ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1991,siku hii inaongozwa na Kituo cha kimataifa cha Wanawake tarehe 10 ilichaguliwa rasmi kuwa siku ya kilele cha maadhimisho haya ikiambatana na siku ya haki za binadamu duniani.[2][1]

Tangu mwaka 1991, zaidi ya asasi 6,000 na zaidi ya nchi 187 hushiriki katika maadhimisho haya. [3]

Maadhimisho hariri

Siku hizi 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huambatana na siku mbalimbali ambazo huadhimishwa ndani ya siku kumi na sita za mwezi Novemba na Desemba.

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 16 days of activism. UN Women www.unwomen.org. Iliwekwa mnamo 6 December 2014.
  2. WHO | 16 Days of Activism Against Gender Violence.
  3. About (en-US). Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-10-29. Iliwekwa mnamo 2020-12-03.
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.