Simoni wa Kurene (kwa Kiebrania שמעון, Šimʿon au Šimʿôn) alikuwa Myahudi kutoka Kurene, Libya, aliyelazimishwa na askari kumsaidia Yesu kubeba msalaba hadi Kalivari, inavyoshuhudiwa na Injili Ndugu zote tatu.[1]

Kituo cha tano cha Njia ya Msalaba, Kanisa kuu la Dubuque, Iowa, Marekani.

Kati ya Wainjili, Marko anamtambulisha kama baba wa Aleksanda na Rufo.

Tendo lake linakumbukwa katika kituo cha tano cha Njia ya Msalaba.[2]

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Desemba[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

https://dacb.org/stories/libya/simon/

  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Simoni wa Kurene kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.