Simoni wa Lipnica, O.F.M., kwa Kipolandi Szymon z Lipnicy (Lipnica Murowana, 1437 hivi – Krakov, 18 Julai 1482), alikuwa padri wa shirika la Ndugu Wadogo nchini Polandi.

Sanamu ya Mt. Simoni katika kanisa la Mt. Yosefu huko Muszyna.

Alitangazwa na Papa Innocent XI kuwa mwenye heri tarehe 24 Februari 1685 akatangazwa mtakatifu na Papa Benedikto XVI tarehe 3 Juni 2007.

Sikukuu yake huadhimishwa siku ya kifo chake, tarehe 18 Julai[1].

Maisha hariri

Alizaliwa katika familia yenye imani na maadili ya Ukristo huko Lipnica Murowana, kusini mwa Poland.

Baada ya kusoma katika shule ya parokia, mwaka 1454 alihamia Kraków ili kusoma katika chuo kikuu maarufu, jina lake Jagiellonian Academy.

Kisha kusikiliza hotuba ya Yohane wa Capestrano, alimuomba shauri ili kujiunga na urekebisho wa Wafransisko wa Observansya.

Aliambiwa amalize kwanza masomo, na ndivyo alivyofanya.

Kisha kupata digrii mwaka 1457 aliingia konventi ya Mt. Bernardino kwa ajili ya unovisi.

Alipomaliza masomo ya teolojia, alipata upadirisho mwaka 1465.

Baadaye alijulikana kama mhubiri hodari, akielekeza watu kuheshimu kama yeye Jina takatifu la Yesu.

Alifariki akiwa anahudumia kwa upendo waliopatwa na tauni[2]. Inasemekana alikuwa amemuomba Mungu afe yeye wasife wengine. Kwa vyovyote, alipofariki mwenyewe, ugonjwa huo ulikoma.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.