Sipriani (kwa Kilatini: Thascius Caecilius Cyprianus; 210 hivi - 14 Septemba 258) alikuwa askofu wa Karthago na mwandishi muhimu kati ya Mababu wa Kanisa, ambaye vitabu vyake vya Kilatini viko hadi leo.

Picha ya Mt. Sipriani.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Septemba[1].

Maisha hariri

Alizaliwa mwanzoni mwa karne ya 3 katika eneo la Afrika kaskazini, labda huko Karthago, alipopata elimu na kuwa mhubiri maarufu.

Baada ya kuongokea Ukristo kwa msaada wa padri Sesili (245), alipata mapema kuwa shemasi, padri akachaguliwa kuwa askofu mwaka 249 na hatimaye akawa mfiadini.

Maandishi yake hariri

Yanapatikana katika magombo 3 na 4 ya Patrologia Latina.

Kitabu chake muhimu zaidi ni "De unitate ecclesiae" (Umoja wa Kanisa). Humo aliandika: "Hawezi kuwa na Mungu kama Baba yule asiye na Kanisa kama mama; . . . asiyekusanya katika Kanisa analitawanya Kanisa la Kristo" (vi.); "Hakuna nyumba nyingine kwa waamini isipokuwa Kanisa pekee" (ix.).

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.