Sireno wa Sirmio (pia: Sinero; Ugiriki[1], karne ya 3 - Sirmium, leo nchini Serbia, 302 hivi) alikuwa mtunzabustani Mkristo ambaye alikamatwa kwa kushtakiwa na mwanamke mwasherati aliyeonywa naye kuhusu tabia yake chafu. Hatimaye aliuawa kwa kukatwa kichwa kwa sababu ya imani yake iliyomfanya akatae kuabudu miungu [2] wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano[3].

Mt. Sireno katika kioo cha rangi (dirisha la kati).

Ndiyo maana anaheshimiwa tangu zamani na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 23 Februari[4].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Monks of Ramsgate. “Sirenus”. Book of Saints, 1921. CatholicSaints.Info. 19 February 2017
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/42510
  3. Alban Butler, Paul Burns, Butler's Lives of the Saints (Continuum International Publishing Group, 1998), p. 233.
  4. Martyrologium Romanum
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.