Kuhusu matumizi mengine ya jina hili angalia Sofia (Madagaska)

Sofia katika Bulgaria
Sofia mbele ya milima ya Vitosha

Sofia (Kibulgaria: София) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Bulgaria mwenye wakazi 1,246,791.

Mji uko upande wa magharibi wa Bulgaria kando la mto Iskar mbele ya milima ya Vitosha inayofikia kimo cha mita 2286 . Ni kitovu cha kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni wa nchi.

Sofia ni mji wa kale mianzo yake ni katika karne ya 7 KK. Wakati wa Dola la Roma ilijulikana kwa jina "Serdica" au "Sardica".

Tangu mwaka 809 BK ilikuwa sehemu ya milki ya Bulgaria ikaitwa "Sredec". Jina la Sofia limetumiwa tangu 1329. Asili yake ni katika kanisa la Mt. Sofia (yaani: Hekima takatifu ya Mungu).

Mji ulirudi nyuma chini ya utawala wa milki ya Osmani ulipotwaliwa na jeshi la Kirusi mwaka 1878 ulikuwa na wakazi 20,000 pekee.

Bunge la kwanza la Bulgaria tar. 22 Machi 1879 likatangaza Sofia kuwa mji mkuu wa Bulgaria. Mji ikakua ikafikia lakhi mwaka 1910 na lakhi tatu mwaka 1939.

Baada ya vita kuu ya pili ya dunia idadi ya wakazi ikaendelea kupanda hadi kupita milioni mnamo 1975.

Wakazi walio wengi ni Wakristo Waorthodoksi. Kuna pia Waislamu na Wayahudi.

Picha za Sofia hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sofia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.