Space Jam ni filamu ya 1996 ya Kimarekani, ambayo imechanganya katuni-na-waigizaji wa kweli, yaani, watu. Ndani ya filamu hii anakuja Michael Jordan, Bugs Bunny (sauti yake imeigizwa na Billy West) na wahusika wengine wote wa Looney Tunes. Filamu ilitayarishwa na Ivan Reitman, na kuongozwa na Joe Pytka (upande wa live-action), Tony Cervone, na Bruce W. Smith (upande katuni). Filamu ilitolewa kwenye maukumbi na Warner Bros. Family Entertainment mnamo 15 Novemba 1996. Filamu inachezwa kivingine kwamba kwanini Michael amerudi tena kwenye mpira wa kikapu, mara hii ameshawishiwa na Bugs Bunny na wenzake.

Space Jam
Imeongozwa na Joe Pytka
Imetayarishwa na Ivan Reitman
Joe Medjuck
Daniel Goldberg
Imetungwa na Leo Benvenuti
Steve Rudnick
Timothy Harris
Herschel Weingrod
Nyota Michael Jordan
Bugs Bunny
Wayne Knight
Daffy Duck
Lola Bunny
Theresa Randle
Bill Murray
Muziki na James Newton Howard
Imesambazwa na Warner Bros.
Imetolewa tar. 15 Novemba 1996 (Marekani)
Ina muda wa dk. Dakika 88
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu Dola za US. 80,000,000 US (makadirio)
Mapato yote ya filamu Dola za US. 230,418,342

Hadithi hariri

Akiwa kama nyota wa NBA Michael Jordan amestaafu kucheza mpira wa kikapu ili mradi kujiendeleza zaidi katika micheza baseball, Mister Swackhammer, mmiliki wa hifadhi ya nje ya dunia ya "Moron Mountain", anaomba vivutio vipya kwa ajili ya hifadhi yake inayoanguka. Anatuma watumishi wake, "Nerdlucks", kwenda kuwateka Looney Tunes, ambao wanaishi chini kabisa ya uso wa Dunia. Wakina Looney Tunes wakalipiza kisa kwa kushindana na Nerdlucks kwa mchezo wa mpira wa kikapu (wakionekana kama siyo warefu). Kwa kujianda na mchezo huo, wakina Nerdlucks wakarudi Duniani kuja kuiba vipaji vya kina Charles Barkley, Patrick Ewing, Muggsy Bogues, Larry Johnson na Shawn Bradley. Wakina Nerdlucks wakatumia vipaji walivyoiba kuwa "Mijitu ya Kutisha", viumbe virefu kabisa ambavyo wakina Looney Tunes hawana uwezo wa kushinda wao wenyewe. Kuwashinda wale, wakina Looney Tunes wakamwita Michael Jordan na msaidizi wake Stan Podolak. Baada ya punde, mchezo ukaanza kati ya wakina Looney Tunes na ile Mijitu, lakini wakina Looney Tunes wakaumizwa vibaya-vibaya na mtindo wa uchezaji wa fujo wa ile Mijitu, hivyo haiwezekani mpaka Jordan pekee, Bugs, Lola na Daffy wamebaki wakisimama na kuacha akicheza mtu mmoja tu. Bill Murray, huwa marafiki na mtayarishaji wa filamu, ana uwezo wa kuingia katika ulimwengu wa Looney Tunes na kujiunga na kikosi chao, akatwaa kizuizi. Kileleni mwa mchezo, wakina Tunes wakawa wapo chini kwa moja na juu ya Michael Jordan kushinda pointi ya mwisho kwa ajili ya timu yake. Kwa kutumia mkono wake usio-maarufu na -wenye kurefuka, Michael Jordan ameweza kufanikisha kuweka mpira kwenye kikapu na kushinda mchezo huo. Baada ya hapo, wakina Looney Tunes wakamrudisha Michael Jordan katika sayari yake ya Dunia, ambapo alirejesha kipaji kilichoibiwa kwa wamiliki halisi na kurejea kwelikweli kwenye NBA.

Washiriki hariri

Charles Barkley, Patrick Ewing, Muggsy Bogues, Larry Johnson, Shawn Bradley, Ahmad Rashad, Del Harris, Vlade Divac, Cedric Ceballos, Jim Rome, Paul Westphal na Danny Ainge wameonekana kama majina yao kwenye filamu hii. Bebe Drake amecheza kama mfanya kazi wa ndani wa Michael Jordan. Sauti za kina Nerdlucks zilichezwa na Jocelyn Blue (Pound), Charity James (Blanko), June Melby (Bang), Catherine Reitman (Bupkus) na Colleen Wainwright (Nawt); sauti za ile Mijitu zilichezwa na Darnell Suttles (Pound), Steve Kehela (Blanko), Joey Camen (Bang), Dorian Harewood (Bupkus) and T.K. Carter (Nawt). Dan Castellaneta na Patricia Heaton ameuza sura akiwa kama kimwana wa Nerdlucks (kwa kusingizia) alikaa pembeni kabisa wakati wa mchezo wa mpira wa kikapu.

Vibwagizo hariri

Viungo vya nje hariri