Spana ni kifaa cha ufundi kinachotumiwa kugeuza skurubu na nati kwa kuzikaza au kuzifungua.

Seti ya spana.
Spana ya kurekebishwa.

Spana nyingi zinalingana na umbo la kawaida la kichwa cha skurubu na nati yake yenye pande 8. Kimsingi kuna aina mbili:

  • Spana iliyofungwa umbo la mviringo inashika kichwa cha skurubu pande zote. Ni kifaa bora hasa kama skurubu na nati yake zimeshikana sana.
  • Spana wazi lenye umbo la mdomo uliofunguliwa inashika skurubu pande nne kati ya pande sita. Inafaa kugeuza skrubu kwenye kona penye nafasi ndogo isiyoruhusu kutumia spana iliyofungwa.

Spana inatakiwa kulingana kikamilifu na ukubwa wa kichwa cha skrubu au nati yake. Kama spana ni kubwa kidogo au skurubu haina kipimo sanifu kuna hatari ya spana kuteleza na kuharibu kona za kichwa au za nati.

Kuna pia spana za pekee zinazoweza kurekebiswa kulingana na kipimo cha skurubu.

Skurubu za pekee huwa na spana zao.

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.