Stamford Bridge (/ˈstæm.fərd ˈbrɪdʒ /) ni uwanja wa mpira ambao uko Fulham, London, kusini-magharibi mwa Uingereza. Ni uwanja wa nyumbani wa Chelsea F.C.. Uwanja uko ndani ya mali ya Park Moore, pia inajulikana kama Walham Green na ni mara nyingi hujulikana kama The Bridge.

Stamford Bridge

Uwanja huu ulifunguliwa mwaka 1877, na klabu ya London Athletic Club mpaka mwaka 1905, wakati mmiliki mpya Gus Mears alianzisha klabu ya soka ya Chelsea ili kuendelea kubaki katika uwanja huo. Chelsea F.C. wamecheza mechi zao za nyumbani tangu wakati huo. mnamo 1990 walifanya marekebisho na ukarabati uwanjani hapo.

Stamford Bridge umekuwa uwanja wa mechi za kimataifa za timu ya taifa ya Uingereza, fainali za Kombe la FA, nusu fainali ya Kombe la FA na michezo ya Charity Shield. Pia unatumiwa kama uwanja wa michezo mingine kama vile kriketi, mchezo wa raga, speedway, Mbio za Greyhound , baseball na soka la Marekani. Mahudhurio rasmi ya mashabikiyalikua 82,905, kwenye mechi ya ligi kati ya Chelsea na Arsenal tarehe 12 Oktoba 1935.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Stamford Bridge kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.