Sulawesi (jina lake la kale Celebes) ni kisiwa cha Indonesia. Kiko kati ya kisiwa cha Borneo upande wa magharibi na visiwa vya Maluku upande wa mashariki. Eneo la kisiwa ni 174,600 km². Mji mkubwa kabisa kisiwani huitwa Makassar. Mwaka wa 2014 idadi ya watu kisiwani imehesabiwa kuwa 18,455,000.

Kisiwa cha Sulawesi,_Indonesia
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.