Sumbawanga ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Rukwa.

Sumbawanga
Sumbawanga is located in Tanzania
Sumbawanga
Sumbawanga

Mahali pa mji wa Sumbawanga katika Tanzania

Majiranukta: 7°57′36″S 31°37′12″E / 7.96000°S 31.62000°E / -7.96000; 31.62000
Nchi Tanzania
Mkoa Rukwa
Wilaya Sumbawanga Mjini
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 303,986
Soko Kuu la mjini Sumbawanga mwaka 2009

Manispaa hiyo ya Sumbawanga ni mojawapo ya wilaya nne za mkoa wa Rukwa. Wilaya nyingine ni Kalambo, Nkasi, na Sumbawanga Vijijini.

Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 147,483 [1]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 303,986 [2].

Asilimia kubwa ya wakazi wake wanategemea kilimo cha mazao ya chakula na biashara, kama mahindi, alizeti, maharage, ulezi, karanga, na kadhalika.

Kabila maarufu mjini ni la Wafipa wakitumia lugha ya Kifipa.

Marejeo hariri

  1. Tanzania.go.tz/census/districts/sumbawangaurban. Jalada kutoka ya awali juu ya 2003-09-03. Iliwekwa mnamo 2003-09-03.
  2. https://www.nbs.go.tz
  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Rukwa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sumbawanga (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.