Tambiko (kutoka kitenzi "kutamba" au "kutambika") ni utekelezaji wa ada maalumu ili kutuliza mizimu, koma au pepo. Mara nyingi matambiko hufanyika kwa kuambatana na kafara. Baadhi ya makabila huweza kuchinja wanyama, wengine hutumia pombe na kadhalika. Kimsingi kafara linalotolewa katika tambiko hutegemea na kabila.

Matambiko huwa hayakubaliki sana katika dini mbalimbali ila huaminika katika makabila kama mila na desturi za jamii hizo. Kwa mfano, tambiko halifai katika sheria ya dini ya Uislamu kutokana na ushirikina unaopatikana ndani ya tambiko.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.