Tewodros II (takriban 1818 – 13 Aprili 1868) alikuwa mfalme mkuu wa Uhabeshi kuanzia 11 Februari 1855 hadi kifo chake. Alimfuata Yohannes III aliyeuzuliwa naye. Jina lake la kubatizwa lilikuwa Kassa Haile Giyorgis. Ingawa hakuwa mrithi wa ufalme aliwashinda wagombea wote vitani. Waingereza walipovamia Uhabeshi chini ya kamanda ya Robert Napier na kushinda jeshi la Uhabeshi, Tewodros II alijiua. Aliyemfuata ni Tekle Giyorgis II.

Tewodros II
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Uhabeshi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tewodros II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.