Theodora wa Turo (pia: Theodosia; Turo, Foinike, leo nchini Lebanoni, 290 hivi - Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli, 2 Aprili 307) alikuwa msichana Mkristo ambaye katika dhuluma ya kaisari Masimino Daia[1] alijitokea hadharani kupongeza waliokuwa hukumuni kwa sababu ya imani yao akiwaomba wamkumbuke watakapomfikia Bwana[2]. Hivyo yeye pia aliteswa kikatili na askari akatoswa baharini[3][4].

Picha takatifu ya Mt. Theodora.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu bikira mfiadini.

Sikukuu yake huadimishwa tarehe 2 Aprili[5][6].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.