Tuwanyika
Tuwanyika kahawianyekundu (Rhamphiophis rostratus)
Tuwanyika kahawianyekundu (Rhamphiophis rostratus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Lamprophiidae (Nyoka walio na mnasaba na chata)
Oppel, 1811
Nusufamilia: Psammophiinae (Nyoka wanaofanana na nyoka-mchanga)
Jenasi: Rhamphiophis
Peters, 1854
Ngazi za chini

Spishi 3:

Tuwanyika, domotai au nondo ni spishi za nyoka wa jenasi Rhamphiophis katika familia Lamprophiidae. Nyoka hawa ni warefu kiasi: kwa kipeo m 1.5-2.5 kulingana na spishi. Rangi yao ni kijivu, kahawia, pinki, machungwa au nyeupe. Kichwa ni kifupi, pua ndefu na macho makubwa.

Tuwanyika huingia mashimo ndani ya ardhi mara nyingi ili kupumzika au kutafuta mawindo yao: wagugunaji, mijusi, vyura na hata nyoka wengine. Wanaweza kuwinda katika vichaka pia.

Chonge zao ni meno ya nyuma kabisa lakini wanaweza kuingiza sumu waking'ata mtu. Hata hivyo sumu yao haina hatari sana kwa watu; inaweza kusababisha maumivu ya kichwa. Wakikaribishwa hutoroka au wasipoweza wanapanua shingo kwa ukaya na kuinua sehemu mbele ya mwili kama fira.

Spishi hariri

Picha hariri

Marejeo hariri

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tuwanyika kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.