Twitter ilikuwa mtandao wa kijamii wa kutoa huduma ya kutuma vijiujumbe vidogo vinavyoitwa "Tweets" na kushea na watu wanaokufuata. Unamilikiwa na kampuni ya Marekani Twitter, Inc. Watumiaji wanatumia simu za mkononi au kompyuta kutuma na kusoma jumbe. Tweet zinaweza kuwa na maneno yenye urefu wa 140 tu. Hata hivyo mwaka 2017 kampuni hii ilitangaza kuongeza idadi ya urefu wa maneno hadi 280.[1] Maneno haya au jumbe hizi zinaonekana katika ukurasa wa mtumiaji. Tweet hizi aghalabu zinaweza kusomwa na mtu yeyote, lakini mtumaji anaweza pia kuzifanya ziwe faragha. Tweet ambazo ni faragha zinaweza kuonekana kwa wale ambao wanakufuata tu.

Logo ya Twitter kabla ya kubadilishwa kuwa X.

Watumiaji wanaweza kujiandikisha na kutweet kwa watu wengine. Mtindo huo unaitwa following au kufuata, na wanaojiandikisha wanaitwa followers au wafuasi. Mwishoni mwa mwaka wa 2009, watumiaji waliweza kufuata orodha za muumbaji.[2][3]

Watumiaji wanaweza kupokea tweets kwa kutumia wavuti ya Twitter. Vilevile wanaweza kutumia programu pepe ambazo zinafanya kazi na Twitter kwenye simujanja. [4]

Twitter ilianzishwa na Jack Dorsey, Noah Glass, Biz Stone, na Evan Williams mnamo Machi 2006 na kuzinduliwa mnamo Julai mwaka huo huo. Twitter, Inc. ina makao yake makuu San Francisco, California na ina zaidi ya ofisi 25 duniani kote. Kufikia mwaka wa 2012, twitter ilikuwa na watumiaji zaidi ya milioni 100 na walituma tweets milioni 340 kwa siku.[5] Mnamo mwaka wa 2013, ilikuwa mojawapo ya tovuti kumi zilizotembelewa zaidi. Kufikia mwanzoni mwa 2019, Twitter ilikuwa na zaidi ya watumiaji milioni 330.[6]

Historia hariri

Twitter ilianzishwa tarehe 21 Machi mwaka 2006, na Jack Dorsey, Biz Stone, na Evan Williams huko San Francisco, California, Marekani. Jukwaa hilo lilizinduliwa rasmi mwezi Julai mwaka huo huo. Twitter ilipata umaarufu haraka kutokana na muundo wake wa ujumbe mfupi, maarufu kama "tweets," ambayo awali ilikuwa na kikomo cha herufi 140. Kikomo hicho kiliondolewa mnamo Novemba 2017, likiruhusu watumiaji kutuma ujumbe wa herufi 280.

Twitter ilikuwa jukwaa la kwanza kuanzisha mfumo wa kufuatilia (follow) na kuwa na mtiririko wa wakati halisi wa matukio (timeline). Watumiaji wanaweza kutoa maoni kwa kutumia alama ya "@" kwa kumtaja mtumiaji mwingine, na pia kutumia alama ya "hashtag" (#) ili kuchangia katika mazungumzo yanayohusiana na mada fulani.

Tangu kuanzishwa kwake, Twitter imekuwa chombo muhimu cha mawasiliano, kutoa jukwaa la kutoa maoni, kushiriki habari, na kusambaza mazungumzo ya ulimwengu. Imetumika kwa kampeni za kisiasa, mawasiliano ya dharura, na kuleta pamoja watu kutoka maeneo mbalimbali duniani. Pia, imeshuhudia mabadiliko kadhaa kwenye jukwaa hilo, pamoja na marekebisho ya sera na kuboresha kwa vipengele vyake.

Tanbihi hariri

  1. "Twitter will double its character count for most users.
  2. There's a List for That. blog.twitter.com (October 30, 2009). Iliwekwa mnamo February 1, 2010.
  3. Twitter Lists!. help.twitter.com (November 9, 2009). Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-12-22. Iliwekwa mnamo February 1, 2010.
  4. Using Twitter With Your Phone. Twitter Support. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-03-15. Iliwekwa mnamo 2010-06-01. “We currently support 2-way (sending and receiving) Twitter SMS via short codes and 1-way (sending only) via long codes.”
  5. Twitter turns six (en-us). blog.twitter.com. Iliwekwa mnamo 2022-08-11.
  6. Brett Molina and Brett Molina. Twitter overcounted active users since 2014, shares surge on profit hopes (en-US). USA TODAY. Iliwekwa mnamo 2022-08-11.

Viungo vya nje hariri