Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 2004

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 2004 ulikuwa wa 55 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 2 Novemba. Upande wa "Republican Party", Rais George W. Bush (pamoja na kaimu wake Dick Cheney) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" John Kerry (pamoja na kaimu wake John Edwards).

Matokeo hariri

Bush akapata kura 286, na Kerry 251, wakati mchaguzi mmoja akampigia kura Edwards badala ya Kerry. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.