Uchapishaji skrini

Uchapishaji skrini (kwa Kiingereza: screen printing) ni ujuzi wa kurembesha mashati kwa kutumia meshi isipokuwa mahala ambako umeweka stencil. Kifaa kinachoitwa squeegee kilicholowa rangi ambayo ungetaka kwa shati lako hufinywa ili kiloweshe vishimo vya meshi na baadaye kifaa kingine huwekelewa ili shati lipate rangi kwa mtindo ambao unataka.

Historia ya uchapishaji skrini hariri

Uchapishaji skrini ulianza katika nchi ya China wakati wa himaya ya Song miakani 960 hadi 1279 AD. Baadaye ujuzi huu ulichukuliwa na Wajapani ambao waliuendeleza kwa kuuongezea maarifa. Kundi la wachoraji ambao walitengeneza National Serigraphy Society walibuni jina Serigraphy mwakani 1930 ili kuweka tofauti kati ya ujuzi huu wa screen printing na uchapishaji skrini uliokuwa ukifanyika katika makampuni.

Kundi la Printers National Environmental Assistance Centre wanasema kwamba uchapishaji skrini ndio jambo ambalo limekuwa likibadilika na kukengeuka kati ya chapa zote. Hii ni kwa sababu uchapishaji skrini waweza kufanyika kwa kutumia bidhaa tofauti tofauti ambazo zapatikana kwa urahisi. Uchapishaji skrini wa Jifanyie wewe mwenyewe au kwa kimombo DIY screen printing ni jambo lililosambaa sana huku wachapishaji skrini wakiweza kuchapa posta za sinema, kurembesha mashati pamoja na kufanya matangazo ya chapa.

Miaka ya 1960 hadi wa leo hariri

Uchapishaji skrini uliweza kushika mizizi vizuri haswa kwa ubunifu wa msanii Andy Warhol ambaye aliweza kufanya watu wapende uchapishaji skrini wa serigraphy. Warhol aliweza kupigwa jeki katika ubunifu wake na mchapishaji skrini mkuu kwa jina Michel Caza aliyekuwa mwanzilishi mkuu wa Fespa na anayekumbukwa kwa kumchora Marilyn Monroe kwa njia ya uchapishaji skrini.

Msanii Sister Mary Corita Kent aliweza kupata jina kwa uchapishaji skrini wake wa serigraphs miakani 1960 na 1970. Kazi yake ya usanii ilikuwa na miavuli mizuri sana na ilikuwa na maudhui ya siasa zenye uzima, Amani na upendo.

Mbinu za chapa hariri

Cha muhimu katika uchapishaji skrini ni meshi ambayo huvutwa kwa fremu. Meshi hutengenezwa kwa kutumia nguo kama vile niloni au polymer. Meshi lazima ivutwe vizuri na kuna kifaa cha kupima mvuto huu wake kinachojulikana kama tensionmeter. Stencil nayo huandikwa maandishi au mfuno wa pateni ambao mchapishaji angetaka uwepo katika shati lake au kifaa kinachochapishwa.

Vyombo vinanyoweza kuchukua uchapishaji skrini hariri

  • Baluni
  • Nguo
  • Vyombo vya hospitali
  • Mashine za kompyuta
  • Viashiria barabara
  • Mabango ya nguo ya kurembesha nyumba
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.