Udhibiti wa saratani

Udhibiti wa saratani unamaanisha kutibu ugonjwa wa saratani au kansa.

Mgonjwa akiandaliwa kwa matibabu ya Saratani

Saratani inaweza kutibiwa kwa kufanyia upasuaji, tibakemo, matibabu kwa njia ya eksirei, matibabu ya tibamaradhi, matibabu ya monokloni ya kingamwili au njia zingine. Uchaguzi ya matibabu hutegemea mahali uvimbe ulipo na daraja lake na hatua ya ugonjwa huo, pamoja na hali ya jumla ya mgonjwa (hali ya utendaji). Idadi kadhaa ya matibabu ya saratani ya majaribio hayajatengenezwa kikamilifu.

Kuondolewa kikamilifu kwa saratani bila kuharibu sehemu zingine za mwili ndilo lengo la matibabu. Wakati mwingine jambo hili linaweza kutimizwa kwa upasuaji, lakini hulka wa saratani ya kuvamia tishu zilizo karibu au kuenea kwenye maeneo ya mbali kupitia uenezi mdogo sana kiasi kwamba hauwezi kuonekana kwa macho mara nyingi huzuia ufaafu wake. Ufaafu wa tibakemo mara nyingi huzuiwa na kiwango cha kusumisha tishu zingine katika mwili. Mnururisho unaweza pia kuharibu tishu ya kawaida.

Kwa sababu neno "saratani // kansa" linarejelea jamii ya magonjwa,[1][2] hakuna uwezekano wa kuwa na aina moja ya "tiba ya saratani" zaidi ya kuwa na tiba moja ya magonjwa yote ya kuambukiza.[3]

Vizuizi vya Anjiojenesisi viliwahi kufikiriwa kuwa na uwezo wa kutkama matibabu ya "risasi fedha (silver bullet)" yanayoweza kutumiwa katika aina nyingi za saratani, lakini jambo hili halijadhihirika katika utendaji.[4]

Upasuaji hariri

Kinadharia, aina za saratani zisizo za kihematolojia zinaweza kutibiwa kama zitaondolewa kabisa kwa upasuaji, lakini jambo hili huwa haliwezekani kila wakati. Wakati saratani imeenea kwenye maeneo mengine ya mwili kabla ya upasuaji, utoaji kamili kwa kufanyia upasuaji kwa kawaida hauwezekani. Katika muundo wa Halstedia wa jinsi saratani inavyoendelea, uvimbe hukua ndani (ya seli moja), kisha kuenea kwenye limfu nodi, kisha kwenye sehemu zingine za mwili. Jmabo hili limesababisha umaarufu wa tiba za ndani pekee (sehemu iliyoathiriwa) kama vile upasuaji wa saratani ndogo. Hata uvimbe mdogo ulio katika sehemu moja unaendelea kutambulika kama ulio na uwezo wa kuenea.

Mifano ya taratibu za upasuaji wa saratani ni pamoja na mastektomia(upasuaji wa matiti) kwa saratani ya matiti, prostatektomia (upasuaji wa tezi kibofu) kwa saratani ya tezi kibofu, na upasuaji wa saratani ya mapafu kwa saratani ya seli zisizo ndogo za mapafu. Lengo la upasuaji linaweza kuwa ama kuondolewa kwa uvimbe pekee, au sehemu nzima ya mwili / ogani. Seli moja ya saratani haiwezi kuonekana kwa macho lakini unaweza kukua tena na kuwa uvimbe mpya, mchakato uitwao kutokea tena. Kwa sababu hii, mwanapatholojia atachunguza Sampuli iliyotolewa ili kuamua ikiwa ina kiasi kidogo cha tishu zilizo na afya, na hivyo kupunguza uwezekano wa kuwa seli ndogo kabisa za saratani zimesalia katika mgonjwa.

Juu ya kuondolewa kwa uvimbe msingi, upasuaji mara kwa mara ni muhimu kwa kuamua hatua ulipofika ugonjwa, kwa mfano, kuamua kiwango cha ugonjwa huo na kama umeenea hadi limfu nodi za eneo hilo. Uamuzi wa hatua ulipofika ugonjwa ni kiukilia kikubwa cha utambuzi wa ugonjwa na haja ya tiba itakayosaidia.

Mara kwa mara, upasuaji ni muhimu kudhibiti dalili, kama vile kubanwa kwa uti wa mgongo au kuzibwa kwa uchengelele. Jambo hili linajulikana kama matibabu ya kutuliza maumivu.

Matibabu kwa njia ya eksirei hariri

Matibabu kwa njia ya eksirei ni matumizi ya mnururisho wa kuweka ioni ili kuua seli za kansa // saratani na kunywea uvimbe. Matibabu kwa njia ya eksirei yanaweza kupenwa kupitia nje ya mwili kwa kutumia boriti ya nje ya tibaredio (EBRT) au ndani ya mwili kupitia tibaredio ya ndani. Athari za matibabu kwa njia ya eksirei huathiri eneo linalotibiwa pekee. Matibabu kwa njia ya eksirei hujeruhi au kuharibu seli katika eneo linalotibiwa ("tishu lengwa") kwa kuharibu nyenzo za kimaumbile za seli hizo, hivyo basi kuzifanya zishindwe kuendelea kukua na kugawanya. Ingawa mnururisho huharibu seli zilizo na saratani pamoja na zile za kawaida, seli nyingi za kawaida zinaweza kupata nafuu kutokana na madhara ya mnururisho na kufanya kazi vizuri. Lengo la matibabu kwa njia ya eksirei ni kuharibu seli za saratani kwani seli nyingi za saratani zinawezekana, na kwa wakati huo kuzuia madhara kwa tishu zilizo karibu zenye afya. Kwa hiyo, aina hii ya matibabu hutolewa kwa sehemu nyingi, na kuruhusu tishu zenye afya kupata nafuu katikati ya sehemu hizi.

Matibabu kwa njia ya eksirei yanaweza kutumika kutibu karibu kila aina ya uvimbe imara, ikiwa ni pamoja na saratani // kansa ya ubongo, matiti, mlango wa uzazi, zoloto, mapafu, kongosho, tezi kibofu, ngozi, tumbo, uterasi, au sarkomasi yenye tishu laini. Mnururisho pia hutumiwa kutibu lukemia na limfoma. Kipimo cha mnururisho kwa kila eneo hutegemea mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kiwango cha hisi kwa mnururisho cha kila aina ya saratani na kama kuna tishu na viungo vilivyo karibu vinavyoweza kuharibiwa na mnururisho. Kwa hiyo, kama ilivyo na kila aina ya matibabu, matibabu kwa njia ya eksirei yana madhara yake.

Tibakemo hariri

Tibakemo ni matibabu ya saratani kwa madawa ("madawa ya kupigana na saratani") ambayo yanaweza kuharibu seli za saratani. Katika matumizi ya sasa, neno "tibakemo" kwa kawaida hurejelea madawa ya sitotoksiki ambayo kwa jumla huathiri seli zinazojigawanya kwa haraka, tofauti na matibabu lengwa (angalia hapo chini). Madawa ya tibakemo huingilia ugawanyaji wa seli kwa njia mbalimbali zinazowezekana, kwa mfano kupitia kurudiwa kwa DNA au mgawanyo wa kromosomu mpya. Aina nyingi za tibakemo hulenga seli zinazojigawanya kwa haraka na hazilengi seli za saratani pekee, ingawa kiasi fulani cha umaalum kinaweza kuja kutoka na seli nyingi za kansa // saratani kutokuwa na uwezo wa kukarabati uharibifu wa DNA, jambo ambalo seli ya kawaida kwa ujumla zinaweza. Kwa hiyo, tibakemo ina uwezo wa kusababisha madhara kwa tishu zenye afya, hasa zile tishu zilizo na kiwango cha juu cha kubadilishwa (km bitana ya matumbo). Kwa kawaida seli hizi hujitengeneza zenyewe baada ya tibakemo.

Kwa sababu baadhi ya madawa hufanya kazi vyema zaidi yakiwa pamoja kuliko yakiwa peke yake, aina mbilia au zaidi za madawa mara nyingi hupeanwa kwa wakati mmoja. Jambo hili linaitwa "tibakemo iliyochanganywa"; madawa mengi ya tibakemo hupeanwa kwa kuchanganywa.[5]

Matibabu ya baadhi ya lukemia na limfoma yanahitaji matumizi ya dozi ya juu ya tibakemo, na mnururisho wa mwili wote (TBI). Matibabu haya huyeyusha uboho, na hivyo uwezo wa mwili kupona na kujaza damu tena. Kwa sababu hiyo, uboho, au kuvuna seli za shina la damu zilizo pembeni hufanywa kabla ya sehemu ya matibabu inayohusisha uyeyushaji, ili kuwawezesha "kuwaokoa" baada ya matibabu imepewa. Jambo hili linajulikana kama uatikaji wa seli za shina kutoka mwili mmoja. Vinginevyo, seli za shina zinazohusishwa na damu zinaweza kuatikwa kutoka kwa mfadhili asiyehusika lakini aliye na seli zinazofanana (MUD).

Matibabu ya kulenga hariri

Matibabu ya kulenga, ambayo yalianza kupatikan kwa mara ya kwanza katika mwisho wa miaka ya 1990, yamekuwa na athari kubwa katika matibabu ya aina fulani za saratani, na kwa sasa ni sehemu iliyo inayohusisha kazi nyingi ya utafiti. Aina hii ya matibabu inahusisha matumizi ya ajenti maalum kwa ajili ya kuharibu protini za seli za saratani. Madawa madogo yanayolenga molekuli kwa jumla huwa vizuizi vya miliki za vimeng'enya juu ya protini zilizo ndani ya seli za kansa zilizobadilika badilika, zilizo wazi zaidi, au kwa vinginevyo zilizo muhimu. Mifano maarufu ni vizuizi vya tirosini kinasi imatinibu (Gleevec / Glivec) na jefitinibu (Iresa).

Matibabu ya kingamwili ya aina moja ni mkakati mwingine ambapo wakala wa matibabu ni kingamwili ambayo hasa hujifunga kwa protini kwenye uso wa seli za saratani. Mifano ni pamoja na anti-HER2/neu kingamwili ya trastuzumab (Heseptini) inayotumika katika saratani ya matiti, na anti-CD20 kingamwili rituksimabu, inayotumika katika aina mbalimbali za madhara // magonjwa ya Seli-B.

Matibabu ya kulenga pia yanaweza kuhusisha peptidi ndogo kama "vifaa elekezi" ambavyo vinaweza kujifunga kwa uso wa vipokezi vya seli au matriki iliyo nje ya seli iliyoathirika inayozunguka uvimbe. Radionuklidi zilizoambatishwa kwa peptidi hizi (mfano RGDs) hatimaye huua seli ya saratani ikiwa nuklidi itaharibikia katika sehemu zilizo karibu na seli hiyo. Hasa oligo au multima za motifu hizi zinazojifunga zina mvutio mkuu, kwa kuwa zinaweza kusababisha umaarum na shauku bora zaidi za uvimbe.

Matibabu kwa nguvu za mwangaza (PDT) ni matibabu ya kansa yenye awamu tatu na yanayohusisha kihisishamwanga, oksijeni ya tishu, na mwangaza (mara nyingi kwa kutumia leza). PDT inaweza kutumika kama tiba kwa kasinoma ya uso wa seli (BCC) au saratani ya mapafu, PDT pia inaweza kuwa muhimu katika kuondoa athari za tishu zenye madhara baada ya kuondolewa kwa uvimbe mkubwa kupitia upasuaji.[6]

Matibabu kupitia kingamaradhi hariri

 
Kasinoma ya seli za figo (sehemu ya chini kushoto) katika Sampuli ya figo.

Matibabu ya kansa kupitia kingamaradhi yanarejelea mikakati tofauti ya kimatibabu iliyoundwa kuchochea mfumo wa kinga ya mwili wa mgonjwa kupambana na uvimbe. mbinu za kisasa za kuzalisha jibu la kinga dhidi ya uvimbe ni pamoja na matibabu ya kingamaradhi ya BCG yanayowekwa ndani ya mishipa kwa kansa ya kibofu cha mkojo iliyo juu juu, na matumizi ya intaferoni na sitokini zingine kuchochea jibu la kinga katika wagonjwa walio na kasinoma ya seli za figo na melanoma. Chanjo za kuzalisha majibu maalum ya kinga ndizo mada zinazofanyiwa utafiti wa kina katika aina kadhaa za uvimbe, hasa melanoma inayoweza kuua // kudhuru na kasinoma ya seli za figo. Sipuleucel-T ni mkakati unaofanana na chanjo katika majaribio ya baadaye ya kikliniki ya kansa ya tezi kibofu ambapo seli za dendriti kutoka kwa mgonjwa huwekwa kwa peptidi za kibofu zenye asidi fosfati ili kuchochea jibu maalum la kinga dhidi ya seli zilizotokana na kibofu.

Uatikaji wa seli za shina za alojeni hematopoetiki ("uatikaji wa uboho" kutoka kwa mfadhili asiye na jeni zinazofanana) unaweza kuchukuliwa kama aina ya matibabu kwa kutumia kingamaradhi, kwani seli za kinga za mfadhili mara nyingi zitashambulia uvimbe huo katika tukio lijulikanalo kama athari za kipandikizi dhidi ya uvimbe. Kwa sababu hii, HSCT ya alojeni husababisha kuongezeka kwa kiwango cha kutibu kuliko uatikaji wa autolojia katika aina kadhaa za kansa, ingawa madhara pia ni makali zaidi.

Matibabu kwa kingamaradhi yanayohusu seli ambapo seli Asili za Kuua za wagonjwa (NK) na T-Limfositi za sitotoksi (CTL) hutumiwa yamekuwa yakitumiwa katika Ujapani tangu mwaka wa 1990. Seli za NK na CTL kimsingi huua seli za kansa wakati zimekuwa. Matibabu haya hupeanwa pamoja na aina zingine za matibabu kama vile upasuaji, matibabu kwa njia ya eksirei au tibakemo na hujulikana kama Matibabu ya Kuimarisha Kinga ya Aina Moja (Autologous Immune Enhancement Therapy) (AIET)[7][8]

Tiba kwa kutumia homoni hariri

Ukuaji wa baadhi ya saratani unaweza kuzuiwa kwa kutoa au kuzuia homoni fulani. Mifano ya kawaida ya aina za uvimbe zinazoathiriwa na homoni ni pamoja na baadhi ya aina za saratani za matiti na tezi kibofu. Kuondoa au kuzuia estrojeni au testosteroni mara kwa mara ni matibabu muhimu ya ziada. Katika baadhi ya aina za saratani, matumizi ya agonisti za homoni, kama vile projestojeni yanaweza kuwa na manufaa ya kimatibabu.

Vizuizi vya anjiojenesisi hariri

Vizuizi vya anjiojenesisi kuzuia ukuaji mkubwa wa mishipa ya damu (anjiojenesisi) kwamba vivimbe huhitaji ili kuishi. Baadhi ya vizuizi hivi, kama vile bevacizumab, vimekubaliwa na vinatumika kwenye kliniki. Mojawapo ya matatizo makuu ya madawa ya kupambana na anjiojenesisi ni kwamba mambo mengi huchochea ukuaji wa mishipa ya damu katika seli za kawaida au zenye kansa. Madawa ya kupambana na anjiojenesisi hulengo jambo moja tu, hivyo kwamba mambo mengine huendelea kuchochea ukuaji wa mishipa ya damu. Matatizo mengine ni pamoja na njia ya matumizi, kudumisha utulivu // uthabiti na shughuli na kulenga katika mishipa ya uvimbe.[9]

Udhibiti wa dalili hariri

Ingawa udhibiti wa dalili za saratani kwa kawaida haufikiriwi kama matibabu ya moja kwa moja ya kansa, ni kiukilia muhimu cha ubora wa maisha ya wagonjwa wa kansa, na una jukumu muhimu katika uamuzi wa iwapo mgonjwa anaweza kupokea matibabu mengine. Ingawa madaktari kwa ujumla wana ujuzi wa kimatibabu wa kupunguza maumivu, kichefuchefu, kutapika, kuhara, kutokwa na damu na matatizo mengine ya kawaida kwa wagonjwa wa saratani, taaluma mbalimbali na maalum za huduma za kupunguza zimeongezeka hasa katika kukabiliana na mahitaji ya udhibiti wa dalili ya kikundi hiki cha wagonjwa. Jambo hili hasa ni sehemu muhimu ya huduma kwa wagonjwa ambao magonjwa yao hayawezi kutibiwa kwa aina zingine za matibabu. Kwa kuwa matibabu mengi ya saratani huhusisha madhara ambayo kwa kiasi kikubwa hayapendezi // yana kera, mgonjwa aliye na matumaini madogo ya kupata tiba anaweza kuamua kutafuta huduma za kupunguza pekee, na kukwepa matumizi ya matibabu makali zaidi yanayompatia kipindi kirefu cha maisha ya kawaida.

Madawa ya maumivu, kama vile afyuni na oksikodoni, na an, madawa ya kuzuia kichefuchefu na kutapika, hutumika sana katika wagonjwa walio na dalili zinazohusiana na saratani. Madawa bora ya kuzuia kutapika kama vile ondansetroni na analogu, pamoja na aprepitanti yamefanya matibabu ya haraka kuweza kufikiwa zaidi katika wagonjwa wa saratani.

Maumivu sugu kutokana na kansa karibu mara zote huhusishwa na tishu kuendelea kuharibika kutokana na utaratibu wa maradhi au matibabu (yaani upasuaji, matibabu kwa njia ya eksirei, tibakemo). Ingawa daima kuna jukumu la sababu za kimazingira na vurugu zinazoathiri katika mwanzo wa tabia za maumivu, hizi huwa si kwa kawaida sababu kuu za mwanzo wa magonjwa katika wagonjwa walio na maumivu ya saratani. Aidha, wagonjwa wengi walio na maumivu makali yanayohusiana na kansa wanakaribia mwisho wa maisha yao na huduma za kupunguzu dalili hizi zinahitajika. Masuala kama vile shutumu ya kijamii ya kutumia opioidi, hali za kazi na utendaji kazi, na matumizi ya huduma ya afya yanaweza kutokuwa muhimu katika udhibiti wa jumla wa kesi hiyo. Kwa hiyo, mkakati wa kawaida wa kudhibiti maumivu ya kansa ni kweka mgonjwa katika hali ya starehe iwezekanavyo kwa kutumia opioidi na madawa mengine, upasuaji, na hatua zingine za kawaida. Madaktari wamekuwa wakisita kuagiza dawa za kutia usingizi kwa maumivu katika wagonjwa wa kansa isiyotibika, kwa hofu ya kuchangia katika ulevi au kupunguza uwezo wa kupumua. Kikundi cha huduma za kupunguza, kikundi cha hivi karibuni kilichotoka kwenye kile cha hospice, kimesababisha uungaji mkono uliotanda zaidi wa matibabu ya kwanza zaidi ya maumivu kwa wagonjwa wa saratani preemptive.

Uchovu ni tatizo kubwa sana na la kawaida kwa wagonjwa wa kansa, na hivi karibuni tu ndipo limekuwa muhimu vya kutosha kuwafanya wanaonkolojia kupendekeza matibabu, hata kama lina nafasi kubwa katika hali ya maisha ya wagonjwa wengi.

Utafiti hariri

Majaribio ya kikliniki, ambayo pia hujulikana kama utafiti, hufanyia majaribio tiba mpya katika watu walio na kansa. Lengo la utafiti huu ni kupata njia bora za kutibu kansa na kuwasaidia wagonjwa wa kansa. Majaribio ya kikliniki huchunguza aina nyingi za matibabu kama vile dawa mpya, njia mpya za kufanya upasuaji au matibabu kwa njia ya eksirei, michanganyiko mipya wa matibabu, au mbinu mpya kama vile tiba ya jeni.

Majaribio ya kikliniki ni mojawapo ya hatua za mwisho za mchakato wa muda mrefu na wa makini wa utafiti wa kansa. Utafutaji wa matibabu mapya huanza katika maabara, ambapo wanasayansi kwanza hubuni na kuchunguza mawazo mapya. Kama njia inaonekana kuwa na matumaini, hatua inayofuata inaweza kuwa upimaji wa matibabu katika wanyama ili kuona jinsi inavyoathiri kansa katika viumbe hai na kama ina athari zinazodhuru. Bila shaka, matibabu yanayofanya kazi vyema katika maabara au katika wanyama si lazima yafanyekazi vizuri katika watu. Tafiti hufanywa kwa kutumia wagonjwa wa saratani ili kutambua ikiwa matibabu yanayoonyesha uwezo wa kufanya kazi ni salama na bora.

Wagonjwa wanaoshiriki wanaweza kusaidiwa na matibabu wanayoyapokea. Wao hupata huduma za kisasa kutoka kwa wataalamu wa kansa, na wao hupokea ama matibabu mapya yanayofanyiwa majaribio au matibabu bora zaidi ya kawaida yanayopatikana ya kansa wanayougua. Wakati uo huo, matibabu mapya pia yanaweza kuwa na hatari zisizojulikani, lakini kama matibabu mpya yanaonekana kufanya kazi vyema au zaidi zaidi ya matibabu ya kawaida, wagonjwa wa utafiti wanayoyapokea wanaweza kuwa kati ya watu wa kwanza kunufaika. Hakuna thibitisho kwamba matibabu mapya yanayofanyiwa majaribio au matibabu ya kawaida yataleta matokeo mazuri. Katika watoto walio na kansa, utafiti wa majaribio ulipata kwamba wale waliojiunga na majaribio hawakuwa kwa wastani na nafasi ya kuwa katika hali bora au mbaya zaidi ya afya wakilinganishwa na wale waliokuwa wakipokea matibabu ya kawaida; jambo hili linathibitisha kwamba kufanikiwa au kutofanikiwa kwa matibabu ya majaribio hakuwezi kutabirika.[10]

Matibabu ya kukamilishana na ya mbadala hariri

Matibabu ya kukamilishana na mbadala (CAM) matibabu ni makundi tofauti ya mifumo ya huduma, weledi na bidhaa za kimatibabu na afya, ambazo si sehemu ya dawa za kisasa.[11] "Dawa za ziada" zinarejelea njia na vitu vinavyotumika pamoja na dawa za kisasa, wakati "dawa mbadala" zinarejelea michanganyiko inayotumika badala ya dawa za kisasa.[12] Matumizi ya CAM ni jambo la kawaida miongoni mwa watu walio na kansa; utafiti wa mwaka wa 2000 ulipata kwamba asilimia 69 ya wagonjwa wa kansa walikuwa wametumia matibabu ya CAM, angalau mara moja, kama sehemu ya matibabu yao ya kansa.[13] Madawa mengi ya kansa ya kukamilishana na mbadala hayajafanyiwa utafiti au majaribio ya kina. Baadhi ya madawa mbadala ambayo yamechunguzwa na kudhahirishwa kuwa hayafanyi kazi huendelea kuuzwa na kukuzwa.[14]

Katika mimba hariri

Matukio ya kansa kuwepo kwa wakati mmoja na mimba yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa umri wa mama wajawazito[15] , na kutokana na ugunduzi wa kuwepo kwa uvimbe katika mama wajawazito wakati wa majaribio yanayofanywa kabla ya mtoto kuzaliwa.

Matibabu ya kansa yanahitaji kuchaguliwa ili kupunguza madhara kwa mama na mtoto wake. Katika baadhi ya matukio kutolewa kwa mimba kwa sababu za kimatibabu kunaweza kupendekezwa.

Matibabu kwa njia ya eksirei kwa jumla hayawezi kutumika, na daima tibakemo huwa na hatari ya kusababisha kuharibika kwa mimba na ulemavu wa kuzaliwa nao.[15] Ni mambo machache sana yanayojulikana kuhusu madhara yanayosababishwa na madawa kwa mtoto.

Hata kama dawa fulani imechunguzwa na kuonekana kuwa haipiti kondo na kumfikia mtoto, aina zingine za saratani zinaweza kudhuru kondo na kuifanya dawa kupita // kupenyeza.[15] Aina fulani za saratani ya ngozi zinaweza hata enea hadi kwa mwili wa mtoto.[15]

Utambuzi pia hufanywa kuwa mgumu zaidi, kwani tomografia kwa kutumia compyuta haiwezekani kwa sababu ya kipimo chake cha mnururisho kilicho juu. Hata hivyo, upigaji picha kwa kutumia mwangwi wa sumaku hufanya kazi kama kawaida.[15] Hata hivyo, vyombo vinavyohitilafiana haviwezi kutumiwa, kwani huwa vinavuka kondo.[15]

Kutokana na matatizo ya kufanya utambuzi mzuri na matibabu saratani wakati wa ujauzito, njia mbadala ni ama kufanyiwa upasuaji wakati mtoto ametimiza kiwango cha kujitegemea ili kuanza matibabu ya kina zaidi ya kansa, au, kama kansa ni mbaya kiasi kwamba mama hawezi kusubiri kwa muda huo wote, basi mimba hutolewa ili kuitibu kansa hiyo.[15]

Tiba katika tumbo la uzazi hariri

Mimba wakati mwingine hutambuliwa wakati bado uko katika utero. Teratoma ndiyo aina ya kawaida zaidi // hujitokeza sana ya uvimbe wa kijusi, na kwa kawaida huwa si hatari.

Nishati ya "ultrasound" hariri

Nishati ya "ultrasound" inafanyiwa utafiti kama aina ya matibabu.

Marejeo hariri

  1. "What Is Cancer?". National Cancer Institute. Iliwekwa mnamo 2009-08-17. 
  2. "Cancer Fact Sheet". Agency for Toxic Substances & Disease Registry. 2002-08-30. Iliwekwa mnamo 2009-08-17. 
  3. Wanjek, Christopher (2006-09-16). "Exciting New Cancer Treatments Emerge Amid Persistent Myths". Iliwekwa mnamo 2009-08-17. 
  4. Hayden, Erika C. (2009-04-08). "Cutting off cancer's supply lines". Nature 458: 686–687. doi:10.1038/458686b. 
  5. Takimoto CH, Calvo E. " Archived 15 Mei 2009 at the Wayback Machine."Principles of Oncologic Pharmacotherapy" Archived 15 Mei 2009 at the Wayback Machine. katika Pazdur R, Wagman LD, Camphausen KA, Hoskins WJ (Eds) Cancer Management: A Multidisciplinary Approach Archived 4 Oktoba 2013 at the Wayback Machine. 11 ed. 2008.
  6. Dolmans, DE; Fukumura D, Jain RK (Mei 2003). "Photodynamic therapy for cancer". Nat Rev Cancer 3 (5): 380–7. PMID 12724736. doi:10.1038/nrc1071. 
  7. Damodar, S; Terunuma H, Abraham S (Oktoba 2006). "Autologous Immune Enhancement Therapy (AIET) for a Case of Acute Myeloid Leukemia (AML) - Our Experience". PASRM 2006-001.  Check date values in: |date= (help)
  8. Sivaraman, G; Pandian A, Abraham S (Oktoba 2008). "Autologous Immune Enhancement therapy for Advanced Carcinoma of Pancreas-A Case Report". PASRM 2008-004.  Check date values in: |date= (help)
  9. Kleinman HK, Liau G (Julai 2001). "Gene therapy for antiangiogenesis". J. Natl. Cancer Inst. 93 (13): 965–7. PMID 11438554. doi:10.1093/jnci/93.13.965. 
  10. Kumar A, Soares H, Wells R et al. (2005). "Are experimental treatments for cancer in children superior to established treatments? Observational study of randomised controlled trials by the Children's Oncology Group". BMJ 331 (7528): 1295 Extra |pages= or |at= (help). PMC 1298846. PMID 16299015. doi:10.1136/bmj.38628.561123.7C. 
  11. Cassileth BR, Deng G (2004). "Complementary and alternative therapies for cancer". Oncologist 9 (1): 80–9. PMID 14755017. doi:10.1634/theoncologist.9-1-80. 
  12. [31] ^ What is CAM? Kituo cha Kitaifa cha Madawa ya Kukamilishana na Mbadala (National Center for Complementary and Alternative Medicine). Ilirudishwa 3 Februari 2008.
  13. Richardson MA, Sanders T, Palmer JL, Greisinger A, Singletary SE (1 Julai 2000). "Complementary/alternative medicine use in a comprehensive cancer center and the implications for oncology". J Clin Oncol 18 (13): 2505–14. PMID 10893280. 
  14. Vickers A (2004). "Alternative cancer cures: 'unproven' or 'disproven'?". CA Cancer J Clin 54 (2): 110–8. PMID 15061600. doi:10.3322/canjclin.54.2.110. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-06. Iliwekwa mnamo 2010-11-30. 
  15. 15.0 15.1 15.2 15.3 15.4 15.5 15.6 "Krebstherapie in der Schwangerschaft extrem schwierig", Curado, 2009-02-20. Retrieved on 2009-06-06. (German) Archived from the original on 2016-03-06.