Uislamu nchini Senegal

Uislamu kwa nchi


Uislamu ni dini yenye nguvu nchini Senegal. Asilimia 92 ya wakazi wa nchini humo wamekadiriwa kuwa ni Waislamu,[1] sehemu kubwa ya waumini wake ni wale wa dhehebu la Sunni wanaofuata mafundisho ya imamu Maliki wakiwa na athira za Usufi.[2] Uwepo wa Uislamu nchini humo ulianza tangu kunako karne ya 11. Ndugu wa Kisufi walienea na ukoloni wa Kifaransa, huku watu wakibadilika katika misingi ya dini kuliko ile ya utawala wa kikoloni. Nguzo kuu za Usufii ni pamoja na Tijaniyyah, kina Muridiyyah au Wamouridi, na kiasi kidogo, Qadiriyyah na wengi kiasi Layene. Kadiro la asilimia 1 la Waislamu wa huko wanafuata Ahmadiyya.[3]

Marejeo hariri

  1. http://www.africaguide.com/country/senegal/culture.htm
  2. "Tolerance and Tension Islam and Christianity in Sub-Saharan Africa", May 2, 2013. Retrieved on 2016-06-25. Archived from the original on 2013-08-28. 
  3. The World's Muslims: Unity and Diversity. Pew Forum on Religious & Public life (August 9, 2012). Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-10-24. Iliwekwa mnamo August 14, 2012.