Ulumbi, kwa asili ya neno, ni sifa ya matumizi bora ya lugha (tafakari chanzo cha neno katika kitenzi cha Kiswahili: kulumba, yaani kutumia maneno vizuri). Wataalamu mbalimbali wameutumia ulumbi kumaanisha "uhodari wa kutumia lugha ili kufaulisha mawasiliano" (Buliba et al 2006:65) au "sifa ya kutumia maneno mengi" (Wamitila 2003: 291). Wengine lakini wameutumia sawa na uwingilugha, yaani uwezo wa kutumia lugha mbili au zaidi (k.m. TUKI 1990: 41; Massamba 2004: 101).

Chini ya kipengele cha kwanza cha ulumbi, yaani uhodari wa kutumia lugha, kuna umahiri na umilisi.

Chini ya kipengele cha pili cha ulumbi, yaani uwezo wa kutumia lugha nyingi, kuna ujozilugha, ubadilishaji msimbo na diglosia.

Marejeo hariri

  • Buliba, Aswani, Kimani Njogu & Alice Mwihaki 2006, "Isimujamii kwa Wanafunzi wa Kiswahili", Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation
  • Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Wamitila, Kyallo 2003, “Kamusi ya Fasihi – Istilahi na Nadharia”, Nairobi: Focus Books

Tazama pia hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ulumbi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.