Uoni mfupi (kwa Kiingereza: "near-sightedness, short-sightedness au myopia") ni tatizo ambalo jicho hupoteza uwezo wake wa kuona vitu vilivyo mbali. Hali hii ni ya kawaida sana na mara nyingi hutokea kwa watu wa familia moja.

 Uoni mfupi
Jedwali la uoni mfupi.

Inatokea wakati lenzi inakuwa na umbo la kupinda sana kusiko kwa kawaida, au wakati jicho ni refu kupita kiasi, hivyo mwanga unaoingia kwenye jicho huzingatia hatua mbele ya retina, badala ya kuingia kwenye retina. Hii inafanya vitu vya mbali kutoonekana vizuri.

Uoni mfupi wa ghafla unaweza mara nyingi kuwa dalili ya kwanza ya ugonjwa wa kisukari cha aina ya pili.

Mara nyingi, inaweza kutibiwa kwa urahisi kwa kutumia miwani au upasuaji.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uoni mfupi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.