Uraia ni hali ya mtu kutambulika chini ya sheria kama mwananchi mwenye haki zote katika nchi fulani. Mtu huyohuyo pengine anaweza kuwa raia wa nchi zaidi ya moja. Hata hivyo kuna watu wasio na uraia wa nchi yoyote.

Mtu anapata uraia kufuatana na sheria za nchi husika. Kwa kawaida ni kwa sababu wazazi wake ni raia wa nchi hiyo naye amezaliwa nchini humo. Lakini si hivyo kila mara, kwa sababu anaweza kuwa na wazazi raia wa nchi tofauti, au anaweza kuzaliwa nje ya nchi yao. Pengine wazazi wenyewe hawakuzaliwa katika nchi ambayo wana uraia wake.

Sheria zinaweza kukubali uraia kwa msingi wa:

  • uraia wa wazazi wote au mmojawapo
  • kuzaliwa nchini
  • kuoana na raia
  • kuandikishwa baada ya kuishi nchini muda mrefu

Mara chache sheria inazuia watu kupewa uraia kwa msingi wa dini n.k.

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uraia kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.