Useremala (kutoka neno la Kiajemi na la Kiarabu) ni aina ya ufundi ambao kimapokeo uilitegemea mbao, lakini siku hizi hata vitu vingine kama metali hutumika[1]. [2].

Vifaa vya kimapokeo vya seremala, Makumbusho ya Cervo, Liguria, Italia.
Maseremala kazini katika kijiji cha India.
Tabaka la maseremala huko Panjab, India (1825)
Kanisa la mbao la karne ya 17 nchini Russia.
Maseremala wa leo kazini.

Seremala hutengeneza vitu mbalimbali kama vile masanduku ya kumwagia zege, milango na madirisha na fremu zake, samani, makabati n.k.

Mara nyingi mtu anajifunza kazi hiyo kwa kusaidia seremala stadi, lakini siku hizi kuna vyuo vingi vinavyofundisha fani hiyo.

Hata upande wa vifaa, badala ya vile vinavyotegemea nguvu ya mikono kama randa, siku hizi wengi wanatumia mashine kama msumeno wa mnyororo maalumu ya kuchania, kunyoosha, kupogoa, kurandia n.k.

Tanbihi hariri

  1. Roza, Greg. A career as a carpenter. New York: Rosen Pub., 2011. 6. Print.
  2. Vogt, Floyd, and Gaspar J. Lewis. Carpentry. 4th ed. Clifton Park, NY: Thomson Delmar Learning, 2006.xvi Print.

Viungo vya nje hariri