Ustaarabu wa Indus

Ustaarabu wa Indus (pia: utamaduni wa Harappa; kwa Kiingereza: Indus Valley civilization) ulikuwa ustaarabu wa Zama za Shaba (3300-1500 KK; kipindi cha kukomaa kikiwa mnamo 2000 KK) [1] uliopatikana katika bonde la mto Indus katika Pakistan na Uhindi ya leo.

Ukubwa na mtandao wa ustaarabu wa Bonde la Indus.

Ugunduzi hariri

Habari zake zimepatikana kwa njia ya uvumbuzi wa kiakiolojia kuanzia miaka ya 1880.

Mji wa kwanza kugunduliwa ulikuwa Harappa iliyoangaliwa na Mwingereza Masson aliyedhani ni mmoja wa miji iliyotembelewa na Aleksanda Mkuu; utafiti wa baadaye ulionyesha umri wake ni wa kale zaidi. Mwanaakiolojia Mhindi R. D. Banerji alitambua mnamo 1923 kwamba mabaki ya Harappa yalifanana na yale ya Mohenjo-daro iliyopo kilomita 600 upande wa kusini. Baada ya kugunduliwa kwa sehemu nyingine yenye maghofu ilionekana kwamba hayo ni mabaki ya ustaarabu ulioanza mnamo mwaka 3000 KK na kuenea katika bonde la mto Indus pamoja na matawimito yake makubwa. Pamoja na miji mingi midogo mabaki ya miji mikubwa mitano yamegunduliwa ambayo ni Harappa, Mohenjo-daro na Ganeriwala katika Pakistan ya leo na Dholavira na Rakhigarhi upande wa Uhindi ya leo.[2].

Miji yake hariri

Ustaarabu huo ulianza wakati wa Zama za Shaba ukaendelea kustawi hadi takriban mwaka 1500 KK. Kwa hiyo ilidumu muda mrefu sana. [3]

Watu wa Bonde la Indus walikuwa wajenzi hodari. Miji yao ilipangwa vizuri. Ilikuwa na mfumo wa majitaka, kwa kuweka mfereji wa majitaka kando ya kila mtaa. Hakuna mifano mingine wa miundombinu hiyo katika sehemu nyingine za Dunia kwa wakati ule. Nyumba zilikuwa na ghorofa moja au mbili, na nyingi zilikuwa na chumba cha bafu lakini kulikuwa pia na bafu za umma. Maji yalipelekwa mjini na kugawiwa kwa matangi ya nyumba. Nyumba zilikuwa pia na choo, na uchafu wa nyumba jirani ulipitishwa kwa kumwaga maji katika mabomba ya kitofali hadi shimo kubwa; mashimo hayo yalisafishwa baada ya muda, labda kwa kutumia yaliyomo kama samadi mashambani.

Tofauti na tamaduni nyingine za milenia ya tatu na ya pili KK katika Misri ya Kale na Mesopotamia hawakuacha majengo makubwa kama mahekalu au majumba ya kifalme. Majengo makubwa zaidi yaliyoweza kutambuliwa yanaonekana kuwa ghala za nafaka.

Maandishi hariri

 
Maandishi ya ustaarabu wa Indus.

Watu walitumia aina ya maandishi lakini hadi leo haijawezekana kuyasoma. Kwa hiyo haijulikani walitumia lugha gani. Mwandiko ulitumia takribani alama 400 na mifano mingi inaonekana kama mabaki ya mihuri iliyoonyesha asili ya bidhaa fulani au yaliyomo ya chombo. Maandishi yote ni mafupi sana yenye alama chache tu.

Mwisho hariri

Haijulikani ni nini kilichosababisha mwisho wa ustaarabu huo. Tangu mwaka 2000 KK kuna dalili za kushuka kwa hali ya uchumi. Mnamo mwaka 1700 KK miji mingi haikukaliwa tena. Utafiti wa masalia ya binadamu kutoka makaburi ya siku zile unaonyesha kuongezeka kwa majeruhi na dalili ya magonjwa kama ukoma na kifua kikuu.[4] Wengine walifikiri ilikuwa labda uhamiaji wa makabila ya Kihindi-Kiulaya walioanza kuingia Uhindi mwisho wa milenia ya pili. Wengine wanaona ilikuwa mabadiliko ya tabianchi hasa kipindi kirefu cha ukame, pamoja na mfululizo wa matetemeko ya ardhi.[5][6].

Picha hariri

Marejeo hariri

  1. Shinde, Vasant.S.; Kim, Y.J.; Woo, E.J.; Jadhav, N.; et, al. (2018). "Archaeological and anthropological studies on the Harappan cemetery of Rakhigarhi, India". PLOS One Volume, 13(2), e0192299. 
  2. Coningham & Young 2015, p. 192. "More than 1,000 settlements belonging to the Integrated Era have been identified (Singh, 2008: 137), but there are only five significant urban sites at the peak of the settlement hierarchy (Smith, 2.006a: 110) (Figure 6.2). These are Mohenjo-daro in the lower Indus plain, Harappa in the western Punjab, Ganweriwala in Cholistan, Dholavira in western Gujarat and Rakhigarhi in Haryana. Mohenjo-daro covered an area of more than 250 hectares, Harappa exceeded 150 hectares, Dholavira 100 hectares and Ganweriwala and Rakhigarhi around 80 hectares each."
  3. Allchin, Bridget 1997. Origins of a Civilization: the prehistory and early archaeology of South Asia. New York: Viking.
  4. Robbins-Schug, G.; Gray, K.M.; Mushrif, V.; Sankhyan, A.R. (November 2012). "A Peaceful Realm? Trauma and Social Differentiation at Harappa". International Journal of Paleopathology 2 (2–3): 136–147. PMID 29539378. doi:10.1016/j.ijpp.2012.09.012.  Check date values in: |date= (help)
  5. Grijalva, K.A.; Kovach, L.R.; Nur, A.M. (1 December 2006). "Evidence for Tectonic Activity During the Mature Harappan Civilization, 2600-1800 BCE". AGU Fall Meeting Abstracts 2006: T51D–1553. Bibcode:2006AGUFM.T51D1553G.  Check date values in: |date= (help)
  6. Prasad, Manika; Nur, Amos (1 December 2001). "Tectonic Activity during the Harappan Civilization". AGU Fall Meeting Abstracts 2001: U52B–07. Bibcode:2001AGUFM.U52B..07P.  Check date values in: |date= (help)

Viungo vya Nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

  Mohenjo-daro travel guide kutoka Wikisafiri

 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ustaarabu wa Indus kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.