Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Utengule Usongwe


Kata ya Utengule Usangu
Majiranukta: 8°41′00″S 33°52′00″E / 8.68333°S 33.86667°E / -8.68333; 33.86667
Nchi Tanzania
Mkoa Mbeya
Wilaya Mbarali
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 19,268
Mahali pa Utengule - Usangu karibu na Chimala.

Utengule Usangu ni kata ya Wilaya ya Mbarali katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 19,268 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,407 [2] walioishi humo.

Msimbo wa posta ni 53607.

Historia hariri

Utengule ilikuwa makao makuu ya Mwene Merere I ambaye katikati ya karne ya 19 aliwaunganisha Wasangu waliowahi kushambuliwa na Wangoni na alifaulu kufundisha mtindo huohuo kwa Wasangu. Huko alijenga boma imara la mawe dhidi ya Wangoni.

Mwanawe Merere II alihamisha makao makuu kwenda Usafwa alipounda Utengule Usongwe baada ya kushambuliwa na Wahehe chini ya Mkwawa. Wakati wa ukoloni wa Wajerumani Wasangu waliambiwa kundoka tena Usafwa wakarudi Usangu.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Mbeya - Mbarali DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2017-03-14. 
  Kata za Wilaya ya MbaraliMkoa wa Mbeya - Tanzania  

Chimala | Igava | Igurusi | Ihahi | Imalilo Songwe | Ipwani | Itamboleo | Kongolo | Lugelele | Luhanga | Madibira | Mahongole | Mapogoro | Mawindi | Miyombweni | Mwatenga | Ruiwa | Rujewa | Ubaruku | Utengule Usangu


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Utengule Usangu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.