Vidonda vya tumbo (kwa Kiingereza: "gastritis") ni miongoni mwa magonjwa ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula katika mwili wa binadamu. Huo ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi sana duniani na huwapata sanasana watu wazima kuliko watoto wadogo.

Mwonekano wa tumbo lenye vidonda.
Dalili za vidonda vya tumbo
Dalili za vidonda vya tumbo

Vyanzo hariri

Chanzo kinaweza kuwa kongosho, tezi inayojihusisha na masuala ya mmeng'enyo wa chakula. Kongosho hutoa baadhi ya vimeng'enya kama asidi ili kusaidia kumeng'enya chakula kwa urahisi lakini inaposhindwa kupima kiasi cha asidi na kuzitoa nyingi mno utaandamwa na vidonda vya tumbo; ndiyo maana unashauriwa kunywa maji mengi. Ni kwamba tindikali hizo zinazopatikana ndani ya tumbo humwagika kwa muda ambao tumbo limezoea kupokea chakula. Mtu anapokaa muda mrefu bila kula tindikali hizo humwagika tu na kukuta tumbo likiwa halina chakula, hivyo huanza kuchubua ukuta wa tumbo. Jambo hili linapotokea mara kwa mara michubuko hiyo huongezeka ukubwa na mwisho huwa vidonda. Kwa hiyo vidonda vya tumbo mara nyingi husababishwa na kutokula chakula kwa wakati unaostahili.

Chanzo kingine cha ugonjwa huo ni mawazo: mtu akiwa na msongo wa mawazo yupo kwenye hatari ya kupata vidonda vya tumbo.

Dalili na tiba hariri

Baadhi ya dalili za ugonjwa huo ni kuwa na maumivu makali ya tumbo, hasa mara ya kula chakula, tumbo kuwaka moto baada ya kula baadhi ya vyakula kama dagaa, mimea ya jamii ya mikunde hasa maharagwe, pia pilipili.

Dalili nyingine ni kizunguzungu, kushindwa kupumua, tumbo kujaa gesi, kufunga choo, kukosa hamu ya tendo la ndoa, kuharibika kwa mimba, homa isiyopona, UTI sugu, choo chenye mchangayiko wa damu, kutapika damu, kupungukiwa damu, maumivu ya mgongo na misuli, kichomi, maumivu ya kichwa, kichefuchefu, kushindwa kula baadhi ya vyakula.

Ugonjwa huo unapozidi kushamiri husababisha pia kupata haja kubwa iliyochanganyika na damu, pia kukosa hamu ya kula chakula na kujisikia kama kutapika pindi tindikali inapokuwa inamwagika tumboni.

Mara nyingi vidonda vya tumbo vinaambatana na chembe ya moyo yaani tumbo linapokusumbua huuma kwa kuambatana na chembe ya moyo na mgonjwa huteseka sana; kwa sababu huo ugonjwa unampangia mgonjwa chakula ambacho awe anakula; akila chakula tofauti mambo yanakuwa mengine.

Endapo mgonjwa hatapata matibabu kwa wakati kutapelekea kutapakaa kwa tindikali mwilini na kunaweza kuwa chanzo cha magonjwa ya kisukari, ini, moyo, figo, ugumba na saratani. Athari kuu ya vidonda vya tumbo vinaposhamiri ni kuwa husababisha kifo.

Kutokana na utafiti wa hapa na pale zimepatikana dawa za kutibu madonda ya tumbo, mojawapo ni asali; hiyo ni dawa nzuri sana kwa vidonda vya tumbo: si hutuliza tu, bali inatibu ukizingatia matumizi. Vilevile ulaji wa bamia na mbogamboga za majani, matunda husaidia kupunguza makali ya vidonda vya tumbo

  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vidonda vya tumbo kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.