Vuguvugu la Uarabuni

Vuguvugu la Uarabuni au Vuguvuru la Kiarabu, Mchipuko wa Uarabuni (Kiarabu: الربيع العربي ‎, kutoka kiing. Arab Spring) ni istilahi iliyokuwa inatumika na vyombo vya habari kwa ajili ya wimbi la mapinduzi la migomo na maandamano yasiyo-na-fujo na yenye-fujo, vurumai, machafuko na vita ya yenyewe kwa wenyewe iliyoanza mnamo tarehe 18 Desemba 2010 katika nchi za Kiarabu.[1]

       Serikali imeondolewa madarakani       Vurumai endelevu za raia wanaodai mabadiliko ya kiserikali       Maandamano na hatimaye mabadiliko ya kiserikali
      Maandamano makubwa kabisa       Maandamano madogo       Maandamano nje ya ulimwengu wa Kiarabu

Watawala waliolazimika kutoka madarakani huko nchini Tunisia, Misri (mara mbili), Libya na Yemen. Machafuko ya kiraia yalitokea huko nchini Bahrain na Syria. Maandamano makubwa katika historia yalitokea huko nchini Algeria, Iraq, Jordan, Kuwait, Morocco na Sudan. Maandamano madogo yalitokea huko nchini Mauritania, Omani, Saudia, Jibuti, Sahara ya Magharibi na Palestina. Kulikuwa na maandamano kiasi kutoka katika nchi ambazo sio sehemu ya Ulimwengu wa Waarabu kama vile Uajemi na Israel.

Kulikuwa na mikinzano huko mipakani mwa nchi ya Israel, na maandamano ya Wakhuzestan wachache wa Kiarabu uliyotokea mwaka 2011. Huko Mali, wapiganaji wa Kituareg wakati wanarudi kutoka katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Libya walichochea mzozo uliotafsiriwa kama sehemu ya "Vuguvugu la Kiarabu"" kwa upande wa nchi za Afrika Kaskazini. Mikinzano ya vikundi vya kimadhehebu iliyotokea huko Lebanoni ilionekana kuchochewa na machafuko ya Syria hivyo basi imechukuliwa kama Vuguvugu la Kiarabu.

Maandamano haya yaliambatana na kampeni za kupinga mambo mbalimbali, migomo, mashambulizi, matembezi ya miguu kwa masafa marefu, vilevile matumizi ya mitandao ya kijamiii kwa kuhamasisha na kuongeza ufahamikaji wa suala lenyewe katika jamii husika katika ulimwengu wa intaneti..

Vuguvugu nyingi za Kiarabu ziliambatana na fujo za kila aina hasa kwa kufuatia mamlaka kutaka kuzuia harakati hizi. Kwa maana hiyo, waandamanaji nao hawakubali kurudi nyuma katika suala zima la kupigania hicho walichokuwa wanakiamini. Msemo mkubwa uliokuwa unatumiwa na wagomaji katika ulimwengu wa Kiarabu ulikuwa Ash-sha`b yurid isqat an-nizam ("watu wanataka kuuangusha utawala wa kidhalimu").[2][3]

Baadhi ya watafiti wamelifananisha suala hili kama zile vuguvugu za mapinduzi yaliyotokea mwaka 1989 huko Ulaya ya Mashariki au Mapinduzi ya 1848 katika majimbo ya Ujerumani.

Kuanza kwa vuguvugu hariri

Mfululizo wa migomo na maandamano katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, ulianzia nchini Tunisia mnamo tarehe 18 Desemba 2010 kwa kufuatia Mohamed Bouazizi kujilipua na mafuta ya taa kwa kupinga manyanyaso na rushwa kutoka kwa maafisa wa polisi. Maandamano haya yaliamsha fujo nyengine nje ya mji ambao tukio hili limetokea na kupelekea fujo na maandamano katika nchi mbalimbali za Kiarabu.

Matukio hariri

Safu hii inaonesha baadhi ya mifululizo ya matukio yaliyotokana na vuguvugu la kwanza la Tunisia kisha kuhamia nchi nyingine za Uarabuni.

  • Desemba 18, 2010:   Tunisia, maandamano yanaanza, baada ya Mohammed kujilipua na moto.
  • Desemba 29, 2010:   Algeria, maandamano yanaanza.
  • Januari 13 16, 2011:   Libya, waandamanaji walidhibitiwa.
  • Januari 14, 2011:   Jordan, maandamano yanaanza.
  • Januari 14, 2011:   Tunisia, serikali imeanguka.
  • Januari 17, 2011:   Oman maandamano madogo yalianza.
  • Januari 18, 2011:   Yemen, maandamano yanaanza.
  • Januari 25, 2011:   Egypt, maandamano yanaanza.
  • Januari 26, 2011:   Syria, mtu mmoja kajitia moto.
  • Januari 28, 2011:   Palestine, maandamano yanaanza.
  • Januari 28, 2011:   Djibouti maandamano madogo yalianza.
  • Januari 30, 2011:   Sudan, maandamano yanaanza.
  • Februari 1, 2011:   Jordan, serikali imeondolewa.
  • Februari 10, 2011:   Egypt, Rais, na makamu wake wamekabidhi madaraka.
  • Februari 10, 2011:   Iraq maandamano madogo yalipangwa. Nouri al-Maliki anatangaza ya kwamba uchaguzi ujao hatogombea.
  • Februari 11, 2011:   Egypt, Rais Hosni Mubarak anajiuzuru.
  • Februari 14, 2011:   Bahrain, maandamano yanaanza.
  • Februari 15, 2011:   Libya kivumbi cha maanadamano kinaanza tena.
  • Februari 19, 2011:   Kuwait, maandamano yanaanza.
  • Februari 20, 2011:   Morocco, maandamano yanaanza.
  • Februari 25, 2011:   Mauritania, maandamano yanaanza.
  • Februari 27, 2011:   Lebanon, maandamano yanaanza.
  • Machi 2011:   Djibouti, maandamano yanaisha.
  • Machi 3, 2011:   Libya kiongozi Muammar Gaddafi anapoteza nguvu ya kuingoza Libya.
  • MachI 5, 2011:   Libya Kikosi cha Anga cha Libya chaanza kulipua miji mikubwa. Upinzani ukalazimika kusanda.
  • Machi 11, 2011:   Saudi Arabia, maandamano yanaanza.
  • Machi 15, 2011:   Syria, maandamano yanaanza.
  • March 19, 2011:   Libya, bombing by foreign air forces began.
  • Aprili 15, 2011:   Iran, maandamano yanaanza.
  • Aprili 18, 2011:   Iran, maandamano yanaisha.
  • Mei 2011:   Oman, maandamano yanaisha.
  • Mei 15, 2011:   Israel, maandamano yanaanza.
  • Juni 5, 2011:   Israel, maandamano yanaisha.
  • Agosti 3, 2011:   Egypt, Kesi ya Hosni Mubarak inaanza.
  • Agosti 21-22, 2011:   Libya Wapinzani nao wameingia mji mkuu Tripoli.
  • Septemba 29, 2011:   Saudi Arabia, chaguzi zilifanyika.
  • Oktoba 20, 2011:   Libya mji wa Sirte, Muammar Gaddafi anauawa na waasi.
  • Oktoba 23, 2011:   Libya, vita ya wenyewe kwa wenyewe inaisha.

Marejeo hariri

  1. Ruthven, Malise (23 June 2016). "How to Understand ISIS". New York Review of Books 63 (11). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 August 2016. Iliwekwa mnamo 12 June 2016.  Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)
  2. Fear and Faith in Paradise. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 February 2017. Iliwekwa mnamo October 23, 2014.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  3. "Arab Winter". America Staging. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 October 2014. Iliwekwa mnamo October 23, 2014.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)