Wabena ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa Njombe, Wilaya za Njombe na Wanging'ombe, lakini pia za Makete na Wilaya ya Ludewa. Mwaka 2001 idadi ya Wabena ilikadiriwa kuwa 670,000 [1].

Lugha hariri

Lugha yao ni Kibena. Kutokana na tahariri ya Dr. Kilemile (2009), Kibena ni lugha tajiri sana kwa maneno na ni pana sana ikiwa na lahaja kuu tano: Ki-Kilavwugi (maeneo ya Ilembula); Kisovi (kuanzia Lusisi hadi Makambako), Kimaswamu (Imalinyi, Njombe mjini na sehemu ya kata ya Mdandu), Ki-Lupembe (Lupembe) na Kimavemba (Uwemba na sehemu ya tarafa ya Igominyi ambayo si ya Maswamu).

Lugha ni moja tu; tofauti ni ndogondogo, zikitokana na matamshi, mfano kukaza "dz", kwa lahaja zote isipokuwa Kikilavwugi ambacho ingawa inaandikwa "dzi" inatamkwa kama "dji" umuhudji; na Kilupembe inaandikwa "dzi" lakini watumiaji wanatamka kama "chi" umuhuchi, achile - amekuja, wakati "adjile" (Kikilawugi)... Wengine wote wanakaza adzile, umuhudzi. Tofauti nyingine ni ya kutumia k na h. Mfano: Kamwene/Hamwene, Kangi?/hangi, ukukulima/uhulima n.k.

Suala lingine ni tofauti ya baadhi ya maneno mfano: Asubuhi: Lwamilawu/palukela; Kuketi: kwikala/hwikala/kutama; Chuma mboga: hukova/kukova imboga na huyava/kuyava imboga; Zizi la Ng'ombe: Ligoma na livaga; nyumbani: hukaye na hunyumba; habari za kazi: mwidaliha na madzengo n.k.

Kamusi inatakiwa kujumuisha maneno yote yanayohitilafiana na kudokeza yanakotumika. Maana kamusi ni kihenge cha lugha. Hivyo kuita kamusi yale maneno machache ya Kibena aliyoorodhesha Dr. Joshua ni dhihaka kwa lugha hii ambayo ni tajiri mno kwa misamiati.

Kwa mfano neno kupiga tu lina maneno zaidi ya 100 yakionyesha huyo aliyepigwa amepigwa wapi na kudokeza hali yake baada ya kupigwa. Pia huashiria hali ya mpigaji. Mfano: (tumia) "k" au "h" kutokana na eneo unalotoka: hutova (general) lakini: hupafula (kiganja), hupefula (nyuma ya kiganja), hututa, hukinya, hung'ilula; hung'alula, hutununa, huwindula, hupwinda, hupana, hulibinga, hufidula, hutadisa, hugong'ola, huniabula, hukinya, huhudugula, huniesa n.k.

  Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wabena (Tanzania) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.