Wangindo ni kabila la watu wanaoishi Kusini mwa Tanzania, katika wilaya ya Liwale na wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Lugha yao ni Kingindo, licha ya kuwa kwa asilimia kubwa ya msamiati na sarufi hurandana na ile ya Kindendeule. Hii ni kwa kuwa Wangindo na Wandendeule chimbuko lao ni moja na walijulikana kama WandondeE.

Wangindo walikuwa warushamishale maarufu na wazuri na walitumiwa sana, hasa na chifu wa Wahehe Mkwawa, alipokuwa akipambana na Wabena na Wasangu.

Wangindo, mbali ya kuishi kusini mwa Tanzania, pia wameenea katika sehemu tofautitofauti za nchi, zikiwemo Zanzibar, Tanga, Morogoro, Mtwara; mfano kijiji cha Mkunya na Mbeya katika kijiji cha Rujewa ambacho inasemekana walipewa na Mkwawa baada ya kumsaidia katika vita vya kikabila.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wangindo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.