Wayback Machine ni tovuti ambayo inatunza kurasa za tovuti za zamani. Inaruhusu kuangalia tovuti ambazo haziko tena au kuangalia maudhui ambayo yamebadilishwa tayari.

Nembo ya Mashine ya Wayback
Muonekano wa Wayback Machine ikionyesha WIkipedia ya Kiswahili na kalenda ambako kumbukumbu imehifadhiwa

Tovuti hiyo hutumia programu za crawler zinazopitia intaneti mara kwa mara na kufanya nakalA za tovuti zinazohifadhiwa kwenye seva ya Wayback Machine. Haitunzi tovuti zote wala mabadiliko yote.

Wayback Machine ilianzishwa mnamo Oktoba 2001 kama sehemu ya Internet Archive ikipatikana kupitia anwani yake.[1] [2]

Marejeo hariri

  1. "Internet Archive launches WayBack Machine". Online Burma Library. 2001-10-25. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-24. Iliwekwa mnamo 2016-03-13. 
  2. "The Internet Archive: Building an 'Internet Library'". Internet Archive. 2001-11-30. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo November 30, 2001. Iliwekwa mnamo 2016-03-14.  Check date values in: |archivedate= (help)