Wilaya ya Kaliua ni moja ya wilaya katika Mkoa wa Tabora, ambayo ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012 kutoka maeneo ya wilaya ya Urambo[1]. Postikodi zake huanza kwa namba 457 [2].

Mahali pa Kaliua katika Mkoa wa Tabora

Eneo hariri

Maeneo ya wilaya hiyo ni kilomita za mraba 14,050. Makao makuu yako kwenye mji wa Kaliua takriban km 125 kutoka Tabora. Wilaya inapakana na Urambo na Wilaya ya Uyui upande wa mashariki, Wilaya ya Mpanda (Mkoa wa Katavi) upande wa kusini, Uvinza na Kibondo (Kigoma) upande wa magharibi. Upande wa kaskazini Wilaya inapakana na Ushetu (Shinyanga) na Bukombe (Geita) upande wa kaskazini-magharibi.

Tabianchi hariri

Tabianchi huonyesha jotoridi baina 16-33, kiwango cha mvua ni ya mm 900-1300 kwa mwaka.

Uchumi hariri

Kilimo cha Kaliua ni mazao kama mahindi, maharagwe, mhoji na viazi vitamu pamoja na tumbaku, karanga, pamba na alizeti halafu asali na mifugo. Sekta ya kilimo huajiri asilimia 80 ya idadi ya watu wa Kaliua.

Tanbihi hariri

Viungo vya Nje hariri

  • [1], tovuti rasmi ya Wilaya
  Kata za Wilaya ya Kaliua - Mkoa wa Tabora - Tanzania  

Ichemba | Igagala | Igombemkulu | Igwisi | Ilege | Kaliua | Kamsekwa | Kanoge | Kashishi | Kazaroho | Kona Nne | Makingi | Milambo | Mkindo | Mwongozo | Nhwande | Sasu | Seleli | Silambo | Ufukutwa | Ugunga | Ukumbi Siganga | Usenye | Ushokola | Usimba | Usinge | Uyowa | Zugimlole