Wilaya ya Mufindi ni wilaya mojawapo kati ya 5 za Mkoa wa Iringa, nchini Tanzania, yenye Postikodi namba 51400.

Mahali pa Mufindi (kijani cheusi) katika mkoa wa Iringa. Wilaya za kusini zimetengwa na kufanywa mkoa mpya wa Njombe.

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 265,829 [1]. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 288,996 [2].

Wilaya imepakana upande wa kaskazini na wilaya za Kilolo na Iringa Mjini, upande wa kusini na mkoa wa Njombe, upande wa mashariki na mkoa wa Morogoro na upande wa magharibi na Mkoa wa Singida.

Mufindi iko sehemu ya Nyanda za Juu za Kusini na sehemu za wilaya ziko mita 2000 juu ya usawa wa bahari. Kwa hiyo kuna baridi na mvua nyingi. Wilayani kuna mashamba makubwa ya chai, misitu ya kupandwa ya Sao Hill inayoongoza kwa kutoa mbao Tanzania na Afrika Mashariki, inastawisha mahindi, maharagwe, viazi, kabichi na pareto.

Baadhi ya vijiji vyake ni: Lwang'a, Udumuka, Ihomasa, Kasanga, Mtambula, Ihegela, Igowole, Ngwazi, Kisasa, Nzivi, Kilolo, Nyololo, Ibatu, Nyakipambo, Ipilimo, Kibao, Mbalamaziwa, Malangali n.k.

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  • www.facebook.com/mufindiradio
  • www.mufindiradio.com
  Kata za Wilaya ya Mufindi - Tanzania  

Idete | Idunda | Ifwagi | Igombavanu | Igowole | Ihalimba | Ihanu | Ihowanza | Ikongosi | Ikweha | Itandula | Kasanga | Kibengu | Kiyowela | Luhunga | Maduma | Makungu | Malangali | Mapanda | Mbalamaziwa | Mdabulo | Mninga | Mpanga Tazara | Mtambula | Mtwango | Nyololo | Sadani


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Mufindi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.