Yohane (kwa Kiitalia Giovanni) Leonardi (Diecimo, 1541Roma, 9 Oktoba 1609) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mwanzilishi wa shirika la Wakleri wa kanuni wa Mama wa Mungu mjini Lucca (Toscana, Italia).

Mt. Yohane Leonardi.
Mt. Yohane Leonardi.

Leonardi alitangazwa na Papa Pius IX kuwa mwenye heri tarehe 10 Novemba 1861, halafu na Papa Pius XI kuwa mtakatifu 1938.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Maisha hariri

Kwanza alifanya kazi kama mfamasia.

Kisha kupewa upadrisho mwaka 1572, alijitosa katika malezi ya vijana parokiani mwake akijiita "Yohane wa Mama wa Mungu".

Mwaka 1574 kama sehemu ya Urekebisho wa Kikatoliki alianzisha kundi lenye juhudi za kiroho la kufundisha imani. Leonardi alitumia kundi hilo kueneza heshima kwa Bikira Maria na desturi ya kuabudu Ekaristi saa arubaini mfululizo.

Baadaye Leonardi alifukuzwa Lucca akahamia Roma akawa rafiki wa mtakatifu Filipo Neri ambaye alimshauri asiende Amerika.

Mwaka 1586 Papa Klementi VIII aliyempa kazi ya kurekebisha monasteri za Wabenedikto wa jamii za Monte Vergine, Vallombrosa na Monte Senario.

Baadaye alianzisha na J. Vivès tapo la kimisionari lililozaa seminari ya Uenezaji wa Imani (kwa Kilatini "Propaganda Fide") ambayo baadaye tena ikawa idara ya Papa kwa umisionari.

Alifariki akihudumia wenzake waliougua influenza iliyoenea Roma.

Urithi hariri

Kundi lake lilikuja kukubaliwa na Papa Paulo V mwaka 1614. Kanuni ya kudumu ilitolewa mwaka 1851.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • "Encyclopédie des Saints et de la Sainteté," Hachette (Kifaransa)

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.