Yohane Mbatizaji Garcia

Yohane Mbatizaji Garcia (Almodóvar del Campo, Ciudad Real, Hispania, 10 Julai 1561 - Cordoba, Hispania, 14 Februari 1613) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Watrinitari, yaani watawa wa Utatu mtakatifu, waliojitoa kabisa kwa ajili ya kukomboa Wakristo waliotekwa utumwani.

Mt. Yohane Mbatizaji Garcia.

Alijitahidi kufanya urekebisho wa shirika hilo kwa kuanzisha tawi la Watrinitari Peku kwa kufuata mfano wa Teresa wa Yesu kati ya vipingamizi vikubwa na tabu nyingi.

Pia aliandika vitabu vingi vya teolojia.

Alitangazwa na Papa Pius VII kuwa mwenyeheri tarehe 26 Septemba 1819, halafu Papa Paulo VI alimtangaza mtakatifu tarehe 25 Mei 1975[1].

Sikukuu yake ni tarehe 14 Februari[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. "Saint John Baptist of the Conception". Santi e Beati. Iliwekwa mnamo 22 July 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.