Yohane Mbatizaji Zhao Mingxi

Yohane Mbatizaji Zhao Mingxi (Beiwangtou, 1844 hivi - Beiwangtou, 3 Julai 1900) alikuwa mlei wa China aliyefia Ukristo wakati wa Uasi wa Mabondia pamoja na kaka yake Petro Zhao Mingzhen.

Wafiadini Wakatoliki wa China.

Bila kujali usalama wao, walikuwa wanajitahidi kusaidia wanawake na watoto Wakristo kukimbia, na ndipo walipouawa[1].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 3 Julai[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/60520
  2. Martyrologium Romanum
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.