Yosefu Benedikto Cottolengo

Yosefu Benedikto Cottolengo (Bra, 3 Mei 1786 - Chieri, 30 Aprili 1842) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki huko Piemonte, leo nchini Italia, aliyetegemea kabisa Maongozi ya Mungu katika huduma zake kwa maskini, wagonjwa na wakiwa wa kila aina alizozitoa katika Nyumba Ndogo ya Maongozi ya Mungu pia kupitia mashirika matatu aliyoyaanzisha ili kuendeleza huduma hizo. Wafuasi wake wanatoa huduma hizo hata Dar es Salaam, Tanzania.

Mtakatifu Cottolengo alivyochorwa na ndugu yake Agostino.

Alitangazwa na Papa Benedikto XV kuwa mwenye heri tarehe 29 Aprili 1917, halafu na Papa Pius XI kuwa mtakatifu tarehe 19 Machi 1934.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Aprili[1].

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
  1. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107