Yoshihide Suga

Mwanasiasa wa Japan na waziri mkuu

Yoshihide Suga (菅 義偉, Suga Yoshihide, amezaliwa 6 Desemba 1948) ni mwanasiasa wa Kijapani anayehudumu kama rais wa Chama cha Kidemokrasia huria, na Waziri Mkuu mteule wa Japani. Uteuzi wake rasmi, umefanyika mnamo 16 Septemba 2020, Suga amekua waziri mkuu mpya wa kwanza wa enzi ya Reiwa[1].

Amewakilisha jimbo la uchaguzi Kanagawa katika Baraza la Wawakilishi la Japani tangu mwaka 1996. Alifanya kazi kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Mawasiliano wakati wa awamu ya kwanza ya Shinzō Abe kama Waziri Mkuu kutoka 2006 hadi 2007, na kama Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri wakati wa awamu ya pili ya Abe kutoka 2012 hadi 2020. Muda wake kama Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri ulikuwa mrefu zaidi katika historia ya Japani. Suga alitangaza kugombea kwake katika uchaguzi wa uongozi wa LDP wa 2020 kufuatia tangazo la Abe la kujiuzulu, na alizingatiwa sana kuwa kiongozi wa kumrithi Abe kama waziri mkuu, baada ya kupata idhini kutoka kwa washiriki wengi wa kura katika chama kabla ya uchaguzi.

Marejeo hariri

  1. "Yoshihide Suga set to become Japan's prime minister after winning LDP election", The Japan Times, 14 September 2020. Retrieved on 14 September 2020. 
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yoshihide Suga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.