Yterbi (Ytterbium) ni elementi ya kimetali yenye alama Yb na namba atomia 70, maana yake kiini cha Yterbi kina protoni 70 ndani yake. Uzani atomia ni 173.045. Katika jedwali la elementi inahesabiwa kati ya lanthanidi na metali za ardhi adimu.

Yterbi (Ytterbium)
Jina la Elementi Yterbi (Ytterbium)
Alama Tb
Namba atomia 70
Mfululizo safu Lanthanidi
Uzani atomia 173.045
Valensi 2, 8, 18, 32, 8, 2
Densiti 6.90 g/cm3
Kiwango cha kuyeyuka °K 1097
Kiwango cha kuchemka °K 1469

Kiasili Yterbi haipatikani kwa hali safi lakini imo ndani ya madini mengi.

Iligunduliwa mnamo mwaka 1878 wakati mwanakemia Mswisi Jean Charles Galissard de Marignac alitenga kutoka ardhi adimu ya "erbia" na kuiita Ytterbia kutokana na kijiji cha Ytterby, Uswidi ambako aliwahi kupata madini aliyochungulia.[1] [2]

Yterbi ni vigumu kutengwa na madini mengine, kwa hiyo haina matumizi mengi isipokuwa viwango vidogo katika leza kadhaa.

Marejeo hariri

  1. Mbali na Yterbi (Yb), kuna pia elementi za Ytri (Y), Erbi (Er) na Terbi (Tb) zilizopokea jina kutokana na kijiji cha Ytterby; elementi za Scandi (Skandinavia), Holmi (Ho, jina la Stockholm), Thuli (Tm, jina la Thule, kisiwa cha kaskazini katika mitholojia ya Kigiriki) ya Scandinavia), na Gadolini (Gd, jina la mvumbuzi Johan Gadolin) zilitambuliwa pia katika madini ya Ytterbi.
  2. Kean, Sam (16 July 2010). "Ytterby: The Tiny Swedish Island That Gave the Periodic Table Four Different Elements". Slate. Iliwekwa mnamo 14 November 2016.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)

Kusoma zaidi hariri

  • Guide to the Elements – Revised Edition, Albert Stwertka, (Oxford University Press; 1998) ISBN 0-19-508083-1

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yterbi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.