Ytterby ni kijiji kwenye kisiwa cha Resarö, katika Manispaa ya Vaxholm kwenye funguvisiwa la Stockholm nchini Uswidi.

Terbiumvägen (terbium Road) na Gruvvägen (Mine Road) karibu na mgodi Ytterby ( 59°25′42″N 18°21′14″E / 59.42836°N 18.35384°E / 59.42836; 18.35384 (Terbiumvägen / Gruvvägen) )

Jina la kijiji linamaanisha "kijiji cha nje". [1] Ytterby ni maarufu kwa sababu katika migodi yake elementi nane zilitambuliwa mara ya kwanza. Elementi nne za Ytri (Y), Yterbi (Yb), Erbi (Er) na Terbi (Tb) zote zimepewa jina la Ytterby.

Ugunduzi wa elementi hariri

Tangu miaka ya 1500 hivi felspar ilichimbwa hapa kwa ajili ya kiwanda cha kauri. Mnamo 1787 luteni Carl Axel Arrhenius aliyechungulia eneo kwa kupata mahali pa kujenga ngome alikuta jiwe jeusi na zito ambalo halikujalikana. [2] Mwaka 1794 jiwe hilo lilifanyiwa utafiti na mtaalamu Johan Gadolin aliyetambua kwamba sehemu kubwa ilikuwa elementi mpya. Mwanakemia wa Uswidi Anders Gustaf Ekeberg alithibitisha ugunduzi huo mwaka uliofuata na akaiita kwa jina la Yttria, na yale madini aliitwa Gadoliniti. [3]

Ndani ya madini ya gadoliniti jumla ya elementi saba ilipatikana.

Mbali na Ytri (Y), Yterbi (Yb), Erbi (Er) na Terbi (Tb), elementi za Scandi (Skandinavia), Holmi (Ho, jina la Stockholm), Thuli (Tm, jina la Thule, kisiwa cha kaskazini katika mitholojia ya Kigiriki) ya Scandinavia), na Gadolini (Gd, jina la mvumbuzi Johan Gadolin) zilitambuliwa katika madini ya Ytterbi. [4]

Marejeo hariri

  1. Emsley, John (2001). Nature's Building Blocks. Oxford University Press. p. 496. ISBN 0-19-850341-5. 
  2. Knutson Udd, Lena (2012). Ytterby gruva (pdf) (Swedish). Fortifikationsverket. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-01-07. Iliwekwa mnamo 6 January 2018.
  3. Krishnamurthy, Nagaiyar (2015). Extractive Metallurgy of Rare Earths (2nd ed.). CRC Press. pp. 2, 839. ISBN 9781466576384. 
  4. Kean (16 July 2010). Ytterby: The Tiny Swedish Island That Gave the Periodic Table Four Different Elements. Slate. Iliwekwa mnamo 14 November 2016.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Uswidi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ytterby kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.