Yucatán ni moja kati ya majimbo 31 ya Mexiko upande wa kusinin-mashariki ya nchi na kaskazini ya rasi ya Yucatán. Ina pwani ndefu na Ghuba ya Meksiko.

Yucatán
Bendera ya Yucatán
Mahali pa Yucatán katika Mexiko

Mji mkuu na mji mkubwa ni Mérida (Kimaya: T'hó' au Ichkanzihóo).

Imepakana na Campeche na Quintana Roo. Kunako mwaka wa 2005, idadi ya wakazi ilikuwa 1,818,948. Eneo la jimbo ni 38,402 km².

Wamaya ni kabila la Yucatán lenye historia ndefu. Mwaka 2009 idadi ya Wamaya ilikadiriwa kuwa 1,200,000 katika jimbo la Yucatán.

Gavana wa jimbo ni Ivonne Ortega Pacheco.

Lugha ni Kihispania na Kimaya.


Miji Mikubwa hariri

  1. Mérida (734,153)
  2. Tizimín (69,553)
  3. Valladolid (68,863)
  4. Progreso (49,454)

Viungo vya Nje hariri

 
Piramidi za Maya, El Castillo, Chichen Itza





  Makala hii kuhusu maeneo ya Mexiko bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Yucatán (jimbo) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.