Zebedayo (kwa Kigiriki Ζεβεδαῖος, Zebedaios, kutoka Kiebrania זְבַדְיָה, Zvad'yah[1], yaani Mwingi au Zawadi yangu[2]), kadiri ya Injili zote nne, alikuwa baba wa Mitume wawili wa Yesu Kristo: Yakobo Mkubwa na Yohane.

Mchoro wa Hans von Kulmbach, Maria Salome na Zebedayo pamoja na wanao Yakobo Mkubwa na Yohane Mwinjili, 1511 hivi.

Injili zinamtaja pia mke wake, Salome[3], ambaye pia alifuatana na Yesu hadi kifo chake msalabani huko Kalivari, nje kidogo ya ngome ya Yerusalemu.

Zebedayo aliishi kwenye Ziwa Galilaya[4] na kuwa mvuvi mwenye wafanyakazi chini yake (Mk 1:19-20; Math 4:21-22; Lk 5:4)[4][5]

Injili zinamtaja pia katika mistari mingine: Math 10:2; 20:20; 26:37; 27:56; Mk 3:17; 10:35; Lk 5:10 na Yoh 21:2.

Baadhi ya wataalamu wanadhani alikuwa pia kuhani.

Tanbihi hariri

  1. Zebedee meaning. Iliwekwa mnamo 13 April 2015.
  2. Topic Bible: Zebedee. Iliwekwa mnamo 13 April 2015.
  3.   "Salome". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
  4. 4.0 4.1 "Zebedee", J. D. Douglas (ed.), The New Bible Dictionary (London: The Inter-Varsity Fellowship, 1963), 1354.
  5. Zebedee. Iliwekwa mnamo 13 April 2015.
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zebedayo kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.