Ziwa la Nasser (kwa Kiarabu بحيرة ناصر, buhairat nāssir) ni bwawa kubwa kwenye mto Nile lililopatikana tangu kufungwa kwa mwendo wa Nile kwa lambo la Aswan nchini Misri kuanzia mwaka 1958.

mtazamo wa paneli wa ziwa nasser
Lake Nasser
Ramani inayoonyesha eneo la ziwa
Anwani ya kijiografia 22°25′N 31°45′E / 22.417°N 31.750°E / 22.417; 31.750Coordinates: 22°25′N 31°45′E / 22.417°N 31.750°E / 22.417; 31.750
Aina ya ziwa Kiegezo
Mito ya kuingia Nile
Mito ya kutoka Nile
Nchi za beseni Egypt, Sudan
Urefu 550 km (340 mi)
Upana 35 km (22 mi)
Eneo la maji 5,250 km2 (2,030 sq mi)
Kina cha wastani 25.2 m (83 ft)
Kina kikubwa 180 m (590 ft)
Mjao 132 km3 ([convert: unit mismatch])[1]
Urefu wa pwani (km) 7,844 km (25,735,000 ft)
Kimo cha uso wa maji juu ya UB 183 m (600 ft)
Marejeo [1]
1 Shore urefu is not a well-defined measure.

Ziwa Nasser liko katika eneo la nchi za Misri na Sudan, hasa kati ya miji ya Aswan (Misri) na Wadi Halfa (Sudan). Eneo lake ni zaidi ya km² 5,200, lina urefu wa kilomita 550 na upana hadi km 35. Mjao hufikia hadi km³ 160.

Jina lilitolewa kwa heshima ya aliyekuwa rais wa Misri Gamal Abdel Nasser aliyefanya azimio la kujenga bwawa.

Faida na matatizo ya ziwa hariri

Kuzuiliwa kwa mwendo wa mto ulimaliza mafuriko ya kila mwaka ya Nile nchini Misri. Kwan upande mwingine matope yenye rutuba hayafiki tena chini ya Aswan na wakulima wanahitaji kununua mbolea wa chumvi waliporidhika zamani na matope yaliyobaki mashambani baada ya mafuriko. Vilevile matope hayo yameanza kujaza nafasi ya ziwa na mjao wake umeendelea kupungua polepole.

Pia delta ya Nile katika Mediteranea haikukua tena lakini imeanza kupungua.

Tanbihi hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa la Nasser kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.