Nyege

Pitio kulingana na tarehe 17:21, 3 Septemba 2017 na Jimmwandishi (majadiliano | michango) (Makala kuhusu libido (uchu wa kujamiana/ngono))
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Libido ni uchu au hamu ya kujamiana ambayo hunapatikana kwa waume na pia kwa wake. Neno hili hutumika sana sana mtu alipo na kiwango cha libido kidogo. Hapo ndipo utakaposikia kwamba fulani ana libido kidogo ama mwanaume fulani amekosa nguvu za kiume. Hata hivyo, yafaa ijulikane kwamba kuna tofauti kati ya hamu ya ngono na nguvu za kiume. Mwanaume asiye na nguvu za kiume huenda akawa na kiasi cha libido kinachofaa lakini hawezi kujamiana na mpenziwe kwa njia inayofaa maana mwili wake hauitikii.

Libido husababishwa na nini

Libido huathiriwa na sababu tofauti kama vile za kibiologia, kisaikologia na za kijamii. Libido huathirikia kibiologia kwa maana homoni za mwili kama vile tesistosteroni na dopamini husababisha mtu awe na uchu wa ngono au akose. Unapokuwa na shida za kisaikologia kama vile huzuni, wasiwasi au jambo linalokusumbua kiakili basi uchu wako wa ngono pia utaenda chini. Kijamii, huenda ikawa kwamba kazi unazozifanya ili kukidhi mahitaji ya kila siku zinakunyima wakati au hata uchu wa ngono. Libido huenda ikaathirika iwapo u mgonjwa maana hutakuwa na uchu au hata fikra za ngono.

Libido na umri

Utafiti umeonyesha kwamba waume huwa na libido ya kiwango cha juu wanapobalehe kati ya umri wa miaka kumi na tano hadi kumi na tisa. Kutoka hapo, libido yao yaenda ikididimia maana homoni ya tesistosteroni pia yafifia. Kwa upande mwingine, wanawake hupata libido ya kiwango cha juu zaidi wanapofikia umri wa miaka thelathini. Ijapokuwa wao huanza tamaa ya ngono wakibalehe, hamu yao huwa juu zaidi wakiwa wenye umri huo wa miaka thelathini.

Dawa za kutitimua libido

Kwa wale walio na libido iliyo chini, kuna madawa ambayo waweza wakapewa na madaktari. Madawa haya huwasaidia kuongezea kiwango cha homoni ya tesistosteroni kama vile testogen,crazy bulk na marine muscle. Kuna vyakula vinavyoongeza libido kama vile ndizi, fig na miparachichi. Matunda haya hujulikana kama aphrodisiacs.

Viungo vya Nje

  1. http://increasetestosterone.review/2017/06/30/testogen-review-debunking-myth-anabolic-testosterone-boosters/
  2. http://increasetestosterone.review/2017/07/01/crazy-bulk-magic-review-worth-money/
  3. http://increasetestosterone.review/2017/06/03/marine-muscle-legal-alternative-to-harmful-steroids/
  4. http://www.healthline.com/health/boost-your-libido-10-natural-tips#1