Upangaji wa harusi
Harusi ni sherehe ya maana sana katika maisha ya binadamu.Siku ya harusi ni siku kubwa sana kwa bwana na bibi harusi ambapo wanajiptata wakiuashi ukapera na kuingia katika ushirika mwingine ambapo watakuwa kitu kimoja. Harusi ni ya maana sana katika jamii za kiafrika ambapo kijana akifikia kuoa huonekana kama mtu mkubwa atakayeweza sana kufanya maamuzi kwa familia yake.
Mwanamke pia huwa na uchu wa kuolewa ili aweze kupata familia yake, kulea watoto na pia kuangalia mumewe.
Mipango ya harusi
Kabla ya siku hii kubwa ya harusi, mipango kabambe hufanywa ili kila kitu kiwe shwari. Kwa jamii nyingi, watu hualikwa ili waweze kuwashuhudia bibi na bwana harusi wakifanya ndoa. Harusi huenda ikafanyika kwa kanisa au hata kwa mku wa wilaya hiyo. Kulingana na wovuti wa Prayer of the Faithful Catholic Wedding, harusi yafaa ipangwe kwa njia sawa sawa.