Ziara

Pitio kulingana na tarehe 06:32, 24 Oktoba 2017 na Jimmwandishi (majadiliano | michango) (ziara)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Ziara ni nomino inayoashiria kutembea au kuzuru mahala fulani. Jina la kizungu la ziara ni trip au travel. Ziara yaweza kufanywa na mtu mmoja au hata kundi la watu. Yaweza kufanyika kwa mbinu tofauti za usafiri kama miguu, baiskeli, gari, gari moshi, meli au hata ndege. Inawezekana pia ukafanya ziara pahala ambapo ni ng'ambo na nchi yako au hata ndani ya nchi yako. Ziara hufanywa na familia sana sana wakati wa likizo wakati watoto wako nyumbani na wazazi wamepewa ruhusa ya kupumzika nyumbani.

Madhumuni ya ziara

Ziara hufanyika kwa sababu tofauti. Waweza ukazuru mahala kwa sababu hizi:

  • Kujifurahisha
  • Kupumzisha akili na mwili
  • Kuona mageni
  • Kujua jamii nyingine na kukagua vile wanavyofanya mambo
  • Kuchukua wakati kutengeneza uhusiano na watu wengine wa mahala tofauti

Historia ya Ziara

Zamani ziara zilifanywa kwa minajili ya kutafuta riziki au kwa sababu ya usalama iwapo kwenye upo hamna chakula cha kutosheleza jamii yako au kuna usalama duni. Ziara pia zilifanywa kwa sababu ya biashara za kuchuuza watumwa, bidhaa kama chumvi na mifugo.

Kwa leo hii, ziara hufanywa kwa madhumuni haya lakini watu wamekuwa wakifanya ziara sana sana kwa madhumuni ya raha. Kwa mfano, wazungu hutembea Afrika ili waweze kuona wanyama pori na pia kuangalia jamii za Kiafrika. Watu hutembea nchini Israel ili waweze kusali na kufuata kumbukumbu za Biblia, watu hutembea jijini York, Uingereza kuweza kuona York Minster na The National Railway Museum. Watu hutembea jijini Las Vegas waweze kucheza kamari na kujitosa kwa anasa.

Viungo vya Nje

  1. Things to do in York
  2. Travel
  3. https://en.wikipedia.org/wiki/Trip