Malcolm Bell Wiseman (Mei 23, 1925 - 24 Februari 2019) alikuwa mwimbaji wa muziki wa country wa Marekani.

Mac Wiseman 2008

Maisha ya zamani

hariri

Alizaliwa Mei 23, 1925, huko Crimora, Virginia. [1] Alisoma shule huko New Hope, Virginia, na kuhitimu kutoka shule ya upili mnamo 1943. Alikuwa na ugonjwa wa polio kutokea umri wa miezi sita; [2] kutokana na ugonjwa wake huo, hakuweza kufanya kazi za kawaida na alitumia muda wake mwingi wa utoto kusikiliza rekodi za zamani za muziki. [3] Alisoma katika shule ya Shenandoah Conservatory ya huko Dayton, Virginia, kabla ya kuhamia Winchester, Virginia, mnamo 1960 na kuanza kazi yake ya kuchezesha muziki katika majukwaa huko WSVA-AM Harrisonburg, Virginia . [4]

Safari ya muziki

hariri

Safari yake ya muziki ilianza kama mchezaji wa besi katika bendi ya Cumberland Mountain Folks, bendi ya muziki wa country, ikiwa na muimbaji Molly O'Day . Wakati Lester Flatt na Earl Scruggs walipoondoka kwenye bendi ya Bill Monroe, Wiseman akawa mpiga gitaa wa bendi yao mpya, iitwayo Foggy Mountain Boys . Baadaye alicheza na Bill Monroe Bluegrass Boys.

Mnamo 1951, wimbo wake wa kwanza wa solo, "'Tis Sweet to Be Remembered", ulitolewa. Kulingana na Rolling Stone wimbo huu "ulimpeleka kwenye umaarufu katika muziki ". [3]

Alikuwa mwanzilishi mwenza wa Chama cha Muziki wa country (CMA) .

Marejeo

hariri
  1. "Mac Wiseman, Bluegrass Icon, Dead at 93", February 25, 2019. 
  2. "Country Hall of Fame Taps Ronnie Milsap, Mac Wiseman, Hank Cochran". Rolling Stone. Aprili 22, 2014. Iliwekwa mnamo Aprili 22, 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 "Country Hall of Fame Taps Ronnie Milsap, Mac Wiseman, Hank Cochran". Rolling Stone. Aprili 22, 2014. Iliwekwa mnamo Aprili 22, 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Country, bluegrass great Wiseman, dead at 93", The Tennessean, February 25, 2019.