Maduka ya United Drapery Stores

United Drapery Stores, au UDS, lilikuwa kundi la Uingereza la maduka ya rejareja ya nguo lililokuwa maarufu Uingereza katika miaka ya 1950 hadi 1980.

Historia ya awali

hariri

Kundi hilo lilianzishwa katika mwaka wa 1927 na kutoka kuanzishwa kwake lilitaka kukua kwa kununua kampuni zingine. Kampuni ilianza na maduka 5 katika eneo laLondon,ilipofika mwaka wa 1931 maduka haya yalikuwa yameongezeka kuwa maduka 112 ya rejareja. Katika mwaka wa 1932, lilikuwa limenunua biashara ya Stewart's Clothiers Ltd na kuongeza maduka yake kuwa 232. Maduka mengine thelathini na saba yalikuwa yameongezwa kwa biashara yao katika mwaka wa 1950,kundi hilo liliponunua mnyororo wa maduka ya nguo wa Scotland,Claude Alexander. Mwaka wa 1953,kundi lilifanya upanuzi kubwa kabisa liliponunua kampuni ya Prices Tailors Limited,kampuni ya Leeds ya ushonaji. Prices ilikuwa imeanzishwa katika mwaka wa 1907 na Henry Price ,ikauza nguo chini ya jina la Fifty Shilling Tailors,ilikuwa na maduka 399 nchini kote. Baada ya kununuliwa na UDS,mnyororo wa Prices uliitwa John Collier.

 
Maduka ya Allders yaliyonunuliwa na kampuni ya maduka ya UDS yakanawiri chini ya uongozi wa Bernard na Jack Lyons

Kampuni zilizonunuliwa baadaye

hariri

Katika mwaka wa 1954,UDS ilinunua Alexandre Limited, kampuni iliyokuwa na makao yake Leeds na ilimilikiwa na Bernard na Jack Lyons na familia zao. Bernard Lyons alichukua usimamizi wa sekta za nguo za wanaume na akawa Mwenyekiti na Mkurugenzi Kuu wa kundi hili baadaye. Jack alihamia London na akachukua majukumu mbalimbali katika kundi hili. UDS iliendelea na sera za upanuzi kwa kupitia ununuzi huku wakinunua maduka 27 ya Brooks Brothers katika mwaka wa 1963 na maduka 45 ya mnyororo wa Peter Pell yakinunuliwa katika mwaka wa 1964. Iliripotiwa kuwa katika mwaka wa 1966 pekee, UDS iliuza zaidi ya suti 1,119,000 nchini Uingereza,hii ikaifanya kuwa mojawapo ya kampuni kubwa kabisa kuuza nguo kwa raia wakati huo.Ikishindana na kama Burton's na Hepworth's.

Ununuzi mkubwa wa kundi la UDS ulifanyika katika mwaka wa 1958,mwenyekiti wa wakati huo Joseph Collier aliweza kununua kundi la Allders la maduka ya nguo. Allders ilikuwa imenanza kama duka moja la nguo lililokuwa na makao yake Croydon,iliendelea na kununua baadhi ya maduka mengine ambayo yakaitwa Allder's chini ya uongozi wa Lyons katika miaka ya 1970.

Siku za mwisho za kampuni hii

hariri

Hata hivyo, kampuni pinzani katika biashara ya nguo za wanaume kwa kampuni ya UDS ilikuwa kampuni ya Burton's (ambalo leo ni sehemu katika kampuni ya Arcadia).UDS ilijaribu kununua Burton's mara kadhaa,hasa sana katika mwaka wa 1967. Jaribio hili lilisimamishwa na serikali ya Uingereza kwa kuwa ,serikali ilisema, lilikuwa dhidi ya maslahi ya umma na haliwasaidii.

Familia ya Lyons ilimiliki hisa chache za UDS.Katika mwaka wa 1983,kundi hili lilinunuliwa na Hanson Trust na likagawanywa kuwa dogo dogo. Maduka mengi yaliyokuwa misingi ya UDS ,yakiwa maduka ya Richard Shops ya kuuza nguo za wanawake,yakiuziwa Arcadia.

Marejeo

hariri
  1. ^See Obituary: Jack Lyons, in The Independent (gazeti la London), 20 Februari 2008.
  2. ^Monopolies & Mergers Commission report Ilihifadhiwa 25 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.

Viungo vya nje

hariri