Mafunzo ya vijana
Mafunzo ya vijana ni mafunzo ya kitaaluma yanayohusika na utafiti katika maendeleo,historia,tamaduni,na siasa ya vijana. Mafunzo haya sio tu yapo katika tamaduni za vijana lakini pia mahusiano,kazi na majukumu ya vijana hao ambayo inachukua nafasi kubwa katika jamii.Mafunzo ya vijana yanaimarisha uelewa na uzoefu ambao unatumika kwa kiwango kikubwa na vijana,ambayo kwa ujumla ni kama ishara ya mabadiliko ya kijamii.Mafunzo haya yanahusisha wasomi wa elimu,lugha,historia,dini,sayansi ya jamii,na mambo mengine ya nidhamu katika ubinadamu na sayansi ya jamii.[[1]Watu wengi waliokuwa kwenye miaka kati ya 15-24 mnamo mwaka 2008 waliishi katika nchi zilizoendelea.[[2]]Ufafanuzi wa vijana umetofautina katika mazingira ya kiutamaduni.[[3]]Uzoefu wa kijamii na mpangilio wa muda na nafasi ni mambo ya muhimu katika mafunzo ya vijana.Wasomi wanaonyesha ni jinsi gani utandawazi na mfumo wa leo wa maisha umeathiri mfumo wa maisha wa vijana ukitofautisha na vizazi vilivyopita.[[4]][[5]]
Marejeo
hariri- ↑ Furlong, Andy (2013). Youth Studies: An Introduction. Routledge. uk. 4. ISBN 978-0-415-56479-3.
- ↑ Furlong, Andy (2012). Youth Studies: An Introduction. Routledge. uk. 227. ISBN 978-0-415-56479-3.
- ↑ Furlong, Andy (2012). Youth Studies: An Introduction. Routledge. uk. 227. ISBN 978-0-415-56479-3.
- ↑ Vandegrift, Darcie (2015). "'We don't have any limits': Russian young adult life narratives through a social generations lens". Journal of Youth Studies.
- ↑ Woodman, Dan; Wyn, Johanna (2015). Youth and Generation: Rethinking Change and Inequality in the Lives of Young People. SAGE publication. uk. 124. ISBN 978-1-4462-5905-4.